DIWANI : WANANCHI TUSHIRIKIANE KUWABAINI WALIOHUSIKA KUMUUA KWA KUMKATA MAPANGA DAKTARI ISAACK
Na Dinna Maningo, Tarime
DIWANI wa Kata ya Kemambo- Nyamongo wilaya ya Tarime mkoani Mara, Rashid Bogomba amewasihi wananchi kutoa ushirikiano kuhakikisha wanakamatwa waliohusika kumuua kwa kumkatakata kwa mapanga Dkt. Isaack Daniel Athuman aliyekuwa Daktari wa upasuaji katika kituo cha Afya Kerende.
Akizungumza na DIMA Online Diwani huyo akiwa nyumbani kwa familia ya Marehemu mkoani Singida amelaani vikali kitendo hicho cha uhalifu na kusema kuwa wamempoteza Daktari muhimu aliyekuwa msaada mkubwa katika utoaji wa huduma ya upasuaji kwa wagonjwa.
Diwani wa Kata ya Kemambo- Nyamongo wilaya ya Tarime mkoani Mara, Rashid Bogomba akiwa nyumbani kwa familia ya Marehemu Dkt. Isaack mkoani Singida aliyeuawa kwa kukatwakatwa mapanga Nyamongo- Tarime."Wakati tukio limetokea sikuwepo nilikuwa Dodoma,nipo nyumbani kwa marehemu Singida.Tumempoteza daktari muhimu wa upasuaji katika kituo chetu cha afya Kerende.
"Alikuwa anatoka Kerende akienda Nyangoto senta ndipo akavamiwa na kuuawa. Ni Daktari aliyejitolea sana kuwahudumia wananchi kifo chake ni pigo kubwa kwa jamii.
Diwani huyo amelihimiza Jeshi la Polisi mkoa wa Polisi Tarime Rorya kuhakikisha linawasaka wahusika hadi wapatikane na wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Hata hivyo Halmashauri ya wilaya ya Tarime kupitia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Solomon Shati amesikitika kutangaza kifo cha mtumishi huyo wa Idara ya afya kilichotokea Mei, 03,2023.
Kwa mujibu wa Diwani Bogomba amesema marehemu aliuawa kwa kukatwakatwa mapanga na watu ambao bado hawajajulikana na kisha kupora pikipiki yake.
Marehemu Dkt. Isaack Daniel Athuman wakati wa uhai wakeNyumba ya milele ikiandaliwa kwa ajili ya kumhifadhi Marehemu Dkt. Isaack
Post a Comment