DKT ANETH : WAZAZI WALEENI KATIKA MAADILI WATOTO WENU WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAZAZI nchini ambao watoto wao wamehitimu kidato cha sita kwa mwaka 2023 wametakiwa kuhakikisha wanaendelea kuweka uangalizi kwa watoto wao katika maadili wanapoelekea kwenye masomo ya vyuo vikuu.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dk.Aneth Komba, Mei, 20, 2023 katika mahafali ya 22 ya Kidato cha Sita ya shule ya Sekondari ya Loyola ya Mabibo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dk.Aneth Komba akizungumza katika tukio hilo la wahitimu wa kidato cha Sita shule ya Sekondari ya Loyola ya Mabibo jijini Dar es Salaam mwaka 2023
Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dk.Aneth Komba ?katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wa kidato cha Sita shule ya Sekondari ya Loyola ya Mabibo jijini Dar es Salaam mwaka 2023,
Dkt. Aneth amesema kuwa wanafunzi hao wanapaswa kuendelea kuangaliwa hasa kwenye masuala ya malezi ili waweze kufikia malengo yao ya maisha.
"Wazazi kazi yetu ya kulea haijaishia hapa, tuendelee kuwafuatilia watoto wetu ili waendelee kusoma na kufikia malengo yao "amesema Dk.Komba.
Aidha, Akijibu hotuba iliyotolewa na Mkuu wa shule ya Loyola, Padri Martin Wawelu kuhusiana na rasimu za Sera na Mitaala, Dk.Komba ameeleza kuwa maoni yote ameyapokea na kuwa yatafikishwa katika maboresho ya rasimu hizo na kueleza kuwa maoni yanaendelea kutolewa na kupokelewa hadi tarehe 31/5/2023.
Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dk.Aneth Komba ?katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wa kidato cha Sita shule ya Sekondari ya Loyola ya Mabibo jijini Dar es Salaam mwaka 2023
Naye Mkuu wa shule, Padri Wawelu ameipongeza Serikali kwa maboresho mbalimbali ya Elimu yenye kuleta tija nchini.
Katika mahafali hayo,TET imetoa zawadi ya vitabu vya kiada nakala 60 kwa shule ya Loyola zenye thamani ya Tsh. 865,000 ambapo mkurugenzi huyo ameuomba uongozi wa shule hiyo kuwapa nafasi wanafunzi wote kuweza kupata muda wa kusoma vitabu hivyo ambavyo vitawekwa kwenye maktaba za shule hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dk.Aneth Komba akikabidhi zawadi ya vitabu vya kiad kwa mkuu wa shule ya Loyola, Padri Martin Wawelu
Wanafunzi 89 kati yao Wavulana 53 na Wasichana 36 wameshiriki katika mahafali hayo ambapo ni ongezeko la wanafunzi 15 kwa mwaka jana 2022.
Wanafunzi hao wanafikisha jumla ya Wanafunzi 7,319 waliohitimu toka mahafali ya kwanza shuleni hapo mwaka 1999.
Shule hiyo ni miongoni mwa shule zaidi ya 845 duniani kote zinazoongozwa na Shirika la Yesu, Shirika la Mapadre wa Kanisa Katoliki (yaani Society of Jesus wanaojulikaja kama JESUITS).
Post a Comment