JICHO LA TANZANIA ORGANIZATION KUTOA ELIMU MATUMIZI YA TEHAMA
>> Lengo wananchi watumie Tehama kujipatia kipato
Na Dinna Maningo, Mara
SHIRIKA lisilo la kiserikali la Jicho la Tanzania limedhamilia kuyafikia maeneo mbalimbali yakiwemo ya vijijini ili kutoa elimu kwa wananchi namna ya kutumia simu mahiri (Smartphone) katika kukuza biashara zao kwa njia ya mtandao.
Akizungumza na DIMA Online Mwenyekiti wa Jicho la Tanzania Organization Taifa, Sospeter Ndabagoye amesema Serikali imefanikisha kupeleka huduma ya umeme vijijini, hivyo kuna kila sababu ya kutoa elimu ya matumizi ya tehama kwa watu waishio mjini na vijijini.
Mwenyekiti wa Jicho la Tanzania Taifa, Sospeter Ndabagoye
Amesema kuwa wananchi wa vijijini wengi walishindwa kununua simu hizo kwakuwa walikuwa hawana uhakika wa umeme ulikuwa bado haujafika vijijini.
"Kwa sasa tehama imekuwa ni sehemu ya maisha kwa watanzania wote aliyepo mjini na kijijini tehama inamfikia. Ukijaribu kuangalia mtandao wa simu kwa sasa umefika karibu maeneo mengi ya nchi yetu.
"Lakini pia tumeiona Serikali imekuwa ikizidi kupeleka umeme maeneo mengi karibu yote ya vijijini. Pengine tunaweza kusema tehama haijafika vijijini kwakuwa watu wengi hawana simu kutokana na kwamba hizi simu za kupangusa walishindwa kuzinunua kwasababu hawakuwa na uhakika wa umeme.
Amesema kuwa wapo wananchi wa vijijini wanatumia simu za kisasa lakini hawajui namna gani wazitumie katka kukuza biashara zao kwa njia ya mtandao, isipokuwa wanazitumia katika salamu na kupeana taarifa mbalimbali kwa kupiga simu, kupokea na kutuma sms.
"Tutawaelimisha watu namna gani watumie simu zao kutangaza biashara zao za mazao na matunda kwenye mitandao ya kijamii kama vile Tovuti, Facebook, Twitter, Instagram na mingineyo ili watanzania wazione na wafanye biashara" amesema Sospeter.
Ameongeza kuwa kwa sasa suala la habari, mawasiliano na tehama linaenda kugusa maeneo mengi ya nchi hivyo ni wakati mzuri wananchi wa mjini na vijijini kufahamu matumizi ya tehama katika nyanja mbalimbali.
"Kwa sasa ni kwamba watu wa mjini na Vijijini wanaendelea kupata elimu, shule nyingi za Kata za msingi na sekondari zimejengwa mjini na vijijini na masomo ya Tehama yanafundishwa.
" Vijana hawa wanapomaliza masomo yao wanarudi vijijini wanapoenda wanakuwa tayari wana maarifa, kwahiyo mtu aliyepo kijijini anaweza kusindika mazao yake na matunda alafu akaposti kwenye mitandao mtu aliyepo Arusha na kwingine akayaona na kufanya nae biasara" Amesema Sospeter.
Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa matumizi ya Tehama yakitumika vijijini yatawasaidia waanchi kujiingizia kipato njia inayoweza kuwasaidia watanzania wengi kujiajiri.
>> Jicho la Tanzania Organization ni Taasisi mahususi yenye makao yake makuu jijini Dodoma, iliyosajiliwa kwa namba 00NGO/R/4753 kwaajili ya watanzania wazalendo walioko ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wenye nia ya dhati na thabiti ya kutoa elimu ya Uraia,Utawala bora,Utunzaji wa Madhingira.
Pia elimu ya ukatili wa kijinsia, afya, ujasiriamali,tehama, maadili na uzalendo kwa jamii na kutambua nafasi na mchango wa kila mmoja katika kujiletea maendeleo
Post a Comment