MKURUGENZI HOSPITALI YA MUHIMBILI AWAOMBA WANANCHI KUCHANGIA DAMU
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KATIKA kuelekea maadhimisho ya siku ya kuchangia damu duniani yanayofanyika kila tarehe 14, Juni ya kila mwaka, uongozi wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili (upanga na Mloganzila) umewaomba wananchi kujitokeza kuchangia damu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi amewaomba wananchi kujitokeza kuchangia damu katika hospitali hiyo huduma zinatolewa kuanzia asubuhi mpaka saa 12 jioni.
"Kwa siku moja mahitaji ya Damu ni chupa/ Unit 120- 150, makusanyo yetu kwa siku ni chupa 60-80 tu, hivyo kufanya Hospitali kuwa na upungufu kwenye benki ya damu kila siku.
"Wachangiaji wafike jengo la Maabara Kuu, kitengo cha Damu Salama kinachotazamana na jengo la Magonjwa ya Dharula (Emergency Medicine)".amesema.
Hospitali ya Muhimbili imekuwa ikihudumia watu mbalimbali wa nje na ndani hivyo mahitaji ni makubwa ya damu kwa kila siku.
Post a Comment