HEADER AD

HEADER AD

MGAHAWA WA VYAKULA ASILI VYA BAHARINI WAZINDULIWA TANGA

Na Boniface Gideon, Tanga

MGAHAWA wa ARBAB TANGA SEA FOOD & MORE mkoani Tanga umezinduliwa rasmi Jijini Tanga utakaotoa huduma za vyakula vya asili kwa Watalii wa ndani na nje ya Nchi.

 Mgahawa huo ni wa kwanza kutoa huduma ya vyakula vya asili vinavyotokana  na rasilimali za bahari ya Hindi.

Kwa mujibu wa waandaji wa mgahawa huo wameeleza kuwa utakuwa Mgahawa maalumu kwa asilimia 90 kutoa huduma za vyakula vya viumbe Bahari na umezingatia utamaduni wa Maisha ya Jamii ya Pwani.

Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungumza Juni, 23, 2023 amempongeza mwanzilishi wa Mgahawa huo.

"Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba ( katikati)akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mgahawa wa vyakula vya asili.

"Pia hakuna biashara itakayofungwa iwe ndogo au kubwa na tutahakikisha tunawalinda wafabiashara wote ili waongeza mtaki zaidi" amesema mkuu huyo wa mkoa. 

Pia amepongeza waandaji wa mgahawa huo kwakubuni na kuona fursa za kiuchumi zinazotokana na Rasilimali bahari huku akiwasisiriza kuongeza mitaji zaidi"Amesisitiza Kindamba.

Amewataka wafanyakazi wa mgahawa huo kuzingatia Maadili ya kazi kwakuwa watahudumia Watalii wa ndani na nje,
"Nyie wahudumu mzingatie Maadili ya kazi yenu, tunatarajia kupata huduma nzuri humu lakini kikubwa zaidi muendane na muda katika huduma zenu "Amesema Kindamba.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Arbab Tanga Sea Food & More,Mbwana Kipito amesema haikuwa kazi rahisi hadi kufikia  lengo hilo lakini kwakuwa alikuwa amedhamiria kutimiza ndoto amefanikiwa,

"Niwaombe Vijana wenzangu wasikate tamaa kutimiza ndoto zao,hapa kwenye huu Mgahawa natarajia kuongeza kiwango kikubwa zaidi Cha Ajira kwasasa nimeajiri Vijana zaidi ya 30 lakini Ajira hizo tunatarajia kuongezeka"Alisisitiza Mbwana



No comments