MAONESHO YA WAJASIRIAMALI WANAWAKE YAZINDULIWA, DC TANGA ATIA NENO
Na Boniface Gideon, Tanga
MKUU wa Wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa amezindua maonesho ya Wajasiriamali wanawake mkoani Tanga maarufu TANGA WOMEN yaliyoandaliwa na waandaji wa maonesho hayo kampuni ya Five Brothers Entanglement.
Mkuu huyo wa wilaya hiyo amewataka Wajasiriamali kutumia maonesho hayo kama sehemu ya kutangaza biashara zao na sio kufikiria kuuza tu biashara.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa Akizungumza wakati wa uzinduzi wa maonesho ya biashara ya Tanga Women Gala msimu wa 6.
"miongoni mwenu mkifika kwenye maonesho mnafikiria kuuza mzigo mlionao kwa siku hizo za maonesho, mkimaliza mnasema faida mmepata mwisho wa siku mnaendelea na maisha mengine "Amesisitiza Mgandilwa.
"Tanga Women Gala ni Jukwaa la Wajasiriamali ambalo limekuwa likifanyika kila mwaka kwa lengo la kuhakikisha wanakua na kuinuka kiuchumi kwa kupanua wigo wa kuwakutanisha linaloandaliwa na Kampuni ya Five Brother Intertainment" Amesema.
Mkuu huyo wa wilaya amewataka wabadilike na kuondokana na hali hiyo badala yake watumie kama jukwaa la kutafuta masoko muda wote kwa kujikita kutangaza Biashara zao na sio kuuza tu wakati wa maoyesho.
Baadhi ya Wajasiriamali watakaoshiriki Maonesho ya Biashara ya Tanga women gala msimu wa 6.
Amesema kuwa ana matumaini makubwa kwamba katika msimu huo wa sita wa Tanga Women, Wajasiriamali watakwenda kutengeneza historia kubwa ambayo itakuwa chachu ya kuendelea kuwainua wajasiriamali mkoani humo kukua kiuchumi
“Niwashukuru Tanga Women Gala kwa kazi kubwa mnaoendelea kuifanya tunajua inawezekana wakawa hawana cha kuwalipa lakini dua za wajasiriamali ambao kila siku mnaendelea kuwainua ndio malipo yenu.
“Pamoja na pongezi mimi kama DC wenu niwapongeza kwa mchango wenu kwa jamii ya wana Tanga ni mkubwa, serikali yetu imetengeneza fursa nyingi ikiwemo kutoa wigo kwa wajasiriamali na wafanyabiashara kufanya biashara zao vizuri bila changamoto zozote, kama kiongozi wa wilaya nawapongeza na niwatake muendeee kufanya hivyo hivyo siku zote”Amesema.
Hata hivyo amewataka kuendelea kupanua wigo kwa wajasiriamali ambao kimsingi hawana uwezo wa kufika kwenye maeneo yao kwa kutengeneza utararibu wa namna ya kuweza kuwafikia na kuwatambua ili kuona namna ya kuwasaidia.
“Lakini maonyesho yetu ni ya siku chache ni vema tukajikita kutengeneza masoko baada ya maonyesho sio wakati wa maonyesho ninasema hivyo kwa sababu kwenye wakati huo tunakuwa na siku tatu mpaka tano hivyo tunapaswa kutegeneza kuona mjasiriamali anafanya biashara siku zote za mwaka”Alisema Mgandilwa
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Nasoro Makau amewaambia wadau na Waandishi wa Habari kuwa maonesho hayo mwaka 2023 yanaingia msimu wa 6 tokea kuasisiwa kwake.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Brothers Entanglement Nasoro Makau ( katikati) akikata keki kuashiria kuanza kwa msimu mpya wa Maonesho ya Biashara ya Tanga women gala msimu wa 6.
"Huu ni msimu wa 6 tokea kuasisiwa kwa maonesho haya, hii ni fursa kubwa kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wanawake kutangaza Biashara zao na tunatarajia kupata wafanyabiashara wakubwa kupitia maonesho haya na wapo ambao tayari wameshatoka kupitia monesho haya" Amesema Makau.
Maonesho ya mwaka huu yatafanyika rasmi septemba 27 hadi 30, 2023 yatakayohusisha wafanyabiashara na wajasiriamali zaidi ya 200 kutoka mikoa yote nchini.
Post a Comment