HEADER AD

HEADER AD

MWANDISHI DIMA ONLINE ATEMBELEA MAKAZI YA ALIYEWAHI KUHUSIKA NA BIASHARA YA WATUMWA

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

MWANDISHI wa Habari wa DIMA ONLINE Chombo cha Habari cha mtandaoni Dinna Maningo, akiwa Zanzibar amefanikiwa kutembelea makazi ya aliyewahi kuwa mfanyabiashara ya watumwa nchini na mmiliki wa mashamba makubwa ya karafuu Hamad B. Muhamad Al- Marjebi maarufu (Tippu Tip).

Tippu Tip alizaliwa mwaka 1832 na kufariki 1905 ni mtoto wa kiume Mwarabu aliyekuwa mfanyabiashara katikati ya Tanzania ambapo alimuoa mtoto wa Chifu wa Kinyamwezi.

Tippu Tip alianza kufanya biashara akiwa na umri wa miaka 18 kupitia njia ya kati kuanzia Bagamoyo na alivuka Ziwa Tanganyika na kuingia Mashariki ya Kongo alikoanzisha utawala mkubwa wa kibiashara.


Alikuwa mfanyabiashara wa pembe za ndovu ili kuwapatia wazungu na wamarekani mahitaji ya pembe za ndovu.

Pia alihusika na biashara ya watumwa nchini. Alikuwa na uhusiano wa kibiashara wa karibu na wafanyabiashara kama Tharia Topan.
         Yaliyokuwa makazi ya Tippu Tip-Zanzibar 

Aliwasaidia wavumbuzi wengi akiwemo Henry Morton Stanley (1841-1904) na Wabelgiji kujenga koloni lao la Kongo, na yeye binafsi aliteuliwa kuwa Gavana.

Wakati Mfalme Leopold wa Ubelgiji (1865-1909) alipowashinda waarabu Kongo, Tippu Tip alirudi Zanzibar ambako alimiliki mashamba makubwa ya Karafuu.


Inaelezwa kuwa  Tippu Tip alikuwa na watumwa 10,000. Alijenga nyumba yake ya kifahari kwa marumaru nyeusi na nyeupe sakafuni, mlango ulionakishwa vizuri, na roshani ya juu kwa juu.

Mwanzoni mwa karne ya 20 aliitumia kama hoteli. Alikufa Zanzibar mwaka 1905 na kuzikwa karibu na nyumba yake.

Mwandishi huyo wa Habari  analipongeza Shirika la Kimataifa la Maendeleo na Elimu (IREX) na Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) waliomwezesha kufika Zanzibar.

          Dinna Maningo Mwandishi wa Habari wa DIMA ONLINE 

" Nawashukuru sana IREX na UTPC kwa kunichagua kuwa miongoni mwa Waandishi wa Habari watakaoshiriki mafunzo ya Usalama wa Mwandishi wa Habari anapokuwa akitekekeza majukumu yake ya kazi.

Mafunzo hayo yataanza Juni, 26- 30 katika ukumbi hoteli ya Spice tree by Turaco Zanzibar. 

"Nimefika Zanzibar leo kwa ajili ya kushiriki mafunzo. Nimebahatika kuona nyumba ya Tippu Tip na kufahamu historia yake. Naamini nitajifunza mengi kwa siku hizi nitakazokuwa Zanzibar" amesema Dinna. 





1 comment: