WATAKIWA KUJITOKEZA KUFANYA UCHUNGUZI WA AWALI WA SARATANI
Na Nashon Kennedy, Mwanza
WATANZANIA wametakiwa kujitokeza kwa wingi kufanya uchunguzi wa awali wa saratani ili wakigundulika kuwa saratani wapatiwe tiba hospitali na kwamba aina zote za ugonjwa wa saratani hutibiwa hospitalini pekee na sio kwa waganga wa kienyeji.
Kauli hiyo imetolewa Juni, 4,2023 jijini Mwanza na Meneja wa Ubora na Ubunifu wa Mradi Mtambuka wa Saratani(TCCP) Edina Selestini wakati alipokuwa akizungumza na mashujaa wa saratani wakazi wa jiji la Mwanza na wadau mbalimbali wakati wa maadhimisho ya siku ya saratani duniani.
“ Kule kwa waganga wa kienyeji na tiba za asili kwakweli wengi wanapoteza tu muda na kukomaza ugonjwa”, amesema.
Ameitaka jamii kuepukana na vitu vinavyosababisha saratani kama vile kuepuka unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara na tumbaku uliokithiri na visababishi vingine.
Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza Claudia Kaluri amesema saratani bado ni miongoni mwa magonjwa yanayoongoza duniani kwa kusababisha vifo kwa watu wengi bila kujali umri wala kipato cha mtu.
Amesema takwimu zinaonyesha kuwa katika kila watu 100,000 kuna wagonjwa 76 wapya wa saratani huku vifo vinavyosababishwa na ugonjwa huo vikifikia 68 kwa kila wagonjwa 100.
“ Vifo hivi vinatokana na wagonjwa wengi kufika hospitalini kwa kuchelewa”, amesema.
Mwenyekiti wa Upendo Cancer Foundation Claris Mhimba licha ya kuwashukuru ndugu, jamaa na marafiki walioungana nao kwenye maadhimisho hayo kwa kuwatia faraja wagonjwa na mashujaa wa saratani walioko jijini Mwanza ameitaka jamii kujitokeza mapema ili kushiriki kwenye upimaji wa awali wa saratani.
Amesema wakijitokeza mapema wataweza kuzitambua afya zao na watakaobainika kuwa na saratani itakuwa ni rahisi kutibiwa.
“Sisi tuliosimama hapa leo, tunalinga kusherehekea siku hii ya mashujaa ni kwa sababu tuliwahi kufanyiwa uchunguzi na kutibiwa”, amesema.
Amesema kwa mujibu wa takwimu zilizopo, kati ya wagonjwa 100 wa saratani watu 68 hufariki kwa ugonjwa huo na kwamba wao mashujaa wa saratani wapatao 32 wamebaki kati ya 68 ambao baadhi yao wamefariki dunia kwa ugonjwa wa saratani.
Mkurugenzi wa Kituo Cha watoto wanaougua saratani Cha Iccare Hillary Sued( alitenyoosha mikono) akizungumza na mashujaa wa saratani walipowasili kituoni hapo na zawadi zao.
Amewashukuru wadau mbalimbali kwa kuendelea kuwasaidia ukiwepo mradi Mtambuka wa kudhibiti saratani(TCCP) ambao uliwapatia mafunzo namna ya kukabiliana na ugonjwa wa saratani na kuwawezesha wao kama mashujaa wa saratani kuungana pamoja .
Amewataka wadau mbalimbali katika jamii kuendelea kuihamasisha jamii kutogoopa kwenda kufanyiwa uchunguzi wa awali wa saratani badala ya kuendelea kuamini ushirikina.
“Hebu tuwasaidie kuelewa hili kwa sababu sisi tumepita pale tumeona hali halisi ilivyo, pamoja na kwamba matibabu ni magumu lakini ndio taratibu zake tumepitia hapo na hatimaye tumeweza kusimama mbele ya umma tukishangilia kwamba tumepona”, amesema
Kwa upande wake, Mtalaam wa Mionzi Tiba kwa wagonjwa wa saratani kutoka Idara ya Saratani Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando, Kidaya Bashari amesema changamoto kubwa iliyoko Kanda ya ziwa ni watu kuchelewa kufika hospitalini, ambapo asilimia 70-80 ya wagonjwa wa saratani huenda bugando kutibiwa wakiwa wamechelewa.
Maadhimisho hayo yalianza kwa mashujaa wa saratani kupitia Cancer Foundation kufanya maandamano kwa kushirikiana na wadau na marafiki ambapo wametembelea wagonjwa wa saratani waliolazwa katika wodi ya saratani katika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando.
Pia wamewatembelea wazazi wanaowauguza watoto walio katika Kituo cha Iccare na kuwapa zawadi mbalimbali kwa ajili ya kuwatia moyo na kuwasaidia wakati wakiendelea na matibabu.
Mkurugenzi wa Kituo cha Kulea Watoto wenye saratani kilichoko Bugarika wilayani Nyamagana cha Iccare Tanzania Hillary Sued amewashukuru Upendo Cancer Foundation kwa kuwatembelea wazazi wanaowauguza watoto wenye saratani katika kituo chake na kutoa msaada wa bidhaa, vyakula na vitu mbalimbali kwa ajili ya watoto hao.
Katibu wa Upendo Cancer Foundation Rose Sawika amesema kitendo cha mtu yeyote katika jamii kupima afya yake kwenye uchunguzi wa awali wa saratani na kupokea majibu yake huyo ni shujaa tayari wa saratani.
Sawika amewataka Watanzania kuendelea kujitokeza kjufanya uchunguzi wa awali wa saratani kwa madai kuwa ugonjwa wa saratani ukijulikana mapema unatibika.
Rais wa Lion Club - Mwanza City Mahesh Choudhary ambaye alitoa bidhaa na zawadi kwa watoto wenye saratani,ameitaka jamii kujenga utamaduni wa kupima afya zao.
Ongezea stori hii ya wadau kwenye stori yako
Mmoja wa wazazi anayeuguza mtoto wake Kituoni hapo Daines Kalori ambaye ni mkazi wa Ukerewe mkoani Mwanza anaushukuru uongozi wa Kituo hicho na ule wa hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa kutoa matibabu kwa mwanawe anayeugua saratani ya figo na kwa sasa anaendelea vizuri.
Naye Phares Naftari mkazi wa Kibondo mkoani Kigoma anaushukuru uongozi wa hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa kumtibia mwanawe saratani ya tezi ambaye kwa sasa anaendelea vizuri na matibabu.
Daines Kalori mkazi wa Ukerewe mkoani Mwanza akitoa ushuhuda wa jinsi ambavyo hospitali ya Bugando ilivyomtibu mwanawe saratani ya Figo.
Rais wa Lioni Club kutoka Jiji la Mwanza Mahesh( Choudhary aliye kushoto aliyevaa kikoti Cha nhano akikabidhi vifaa na baadhi ya vitu kwenye Kituo Cha kulea watoto wenye saratani kilichoko Bugarika jijini Mwanza Cha Iccare Tanzania
Rais wa lion kutoka Mwanza City Mahesh Choudhary aliyevaa kizibao Cha nhano akikabidhi mkeka kama sehemu ya vitu alivyowakabidhi watoto wanaougua saratani kituoni hapo.
Post a Comment