HEADER AD

HEADER AD

WAVUTIWA NA FILAMU YA MARRIED TO WORK INAYOTANGAZA UTALII ZANZIBAR

Na Andrew Chale,  Zanzibar

FILAMU ya Married to Work ambayo imeandaliwa katika viunga vya Zanzibar na kuigizwa na wasanii mbalimbali akiawemo Idrissa Sultan imepokelewa kwa mikono miwili na wadau.

Ni katika tamasha la 26 la Filamu la  inchi za Jahazi  (ZIFF), lililoanza Juni 24, na kutarajia kumalizika Julai 2, mwaka huu.

Baadhi ya wadau wamezungumza na Mwandishi wa habari hizi na kuelezea filamu hiyo ambayo imetengezwa ikiwa na lengo ya kutangaza Utalii wa Zanzibar lakini pia inaburudisha.


"Tumeona baadhi ya maeneo ya Zanzibar, lakini pia tumeambiwa ipo katika mtandao mkubwa wa filamu wa Netflix ambao ni maarufu hivyo uwepo wake kule unaendelea kukuza kisiwa chetu na Utalii wake" amesema Yusuf Ali Jumanne mkazi wa Unguja,

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Salha na Aishah wamepongeza filamu hiyo ikiwemo stori yake licha ya kuwa upande wa mahusiano na kwamba inafundisha.

"Nimependa uzuri wa video yenyewe lakini hata maeneo walioenda kuigizia.
Zanzibar yetu itapendeza na tunaomba wasanii waendelee kuja kuigiza maeneo haya" amesema Aishah.

Awali wasanii Idrissa Sultan na Mzee Chillo walipanda katika jukwaa la ZIFF na kutoa neno ya filamu hiyo.

Idrissa amesema kuwa, miongoni mwa vitu vilivyo kwenye filamu hiyo vilimpa ujasiri mkubwa na kuona anakuwa katika tasnia hiyo.


"Wazanzibar ni wema sana, nashukuru sana kwa kunipokea kuja kufanya hii filamu huku, leo hii mmeweza kuipokea na kufurahia." Amesema Idrissa

Aidha,  ameongeza kuwa kupitia utanzania wao wanapaswa kutumia fursa ya kutengeneza filamu bora, lakini pia utayari mkubwa ndio unaozalisha filamu nzuri." Amesema Idrissa.

Kwa upande wake Mzee Chilo ameshukuru wadau wa filamu kwa kuendelea kufuatilia filamu za Tanzania, ambapo amewaomba wasanii kupata wasaha wa kutembelea Zanzibar ilikujifunza vitu vingi zaidi katika tasnia hiyo.




No comments