MBIO ZA NGALAWA ZATIA FORA TAMASHA LA 26 LA ZIFF
Na Andrew Chale, Zanzibar
TAMASHA la Kimataifa la Filamu za Nchi za Jahazi (ZIFF) linaloendelea Unguja-Zanzibar limeendelea kupambwa na shamra shamra mbalimbali ikiwemo mbio za Ngalawa (Mtumbwi wa kitamaduni) ambazo ni miongoni mwa michezo ya asili visiwani hapa inayopendwa na watu wengi toka zamani.
Katika mbio hizo, Ngalawa zaidi 12 ziliweza kushindana kuwania ushindi maalum wa kiasi cha fedha ambapo washiriki uzunguka na Ngalawa hizo bahari ya Hindi.
Akizungumza katika mashindano hayo, Mratibu wa Jukwaa la Wanawake na Vijijini la ZIFF, Sabrina Faraja amesema kuwa washiriki wa Ngalawa hizo hutoka maeneo mbalimbali ya Zanzibar hufika kushindana na kuwania zawadi zinazotolewa kila mwaka na ZIFF.
"Mshindi wa kwanza anakabidhiwa kitita cha fedha, wa kwanza anapata Laki Saba, na wa Pili Laki Tano huku wa Tatu akipata Laki tatu.
Wengine wanapata kifuta jasho kwa ushiriki wao, huku pia zawadi mbalimbali za ushiriki hutolewa.
Aidha, katika mbio hizo, Ngalawa 12 zilizoshindana, Ngalawa moja ilishindwa kuendelea baada ya kupoteza muelekeo wakati wa kuanza kwa mbio hizo na kufanya Ngalawa 11 pekee kumaliza mbio hizo licha ya kuwa na upepo wa wastani baharini.
Ngalawa zilizoshinda ni pamoja na Ngalawa ya Robin Batista nafasi ya kwanza, nafasi ya pili Ngalawa ya WIOMSA na nafasi ya tatu Ngalawa ya AZAM TV.
Ngalawa zingine ni pamoja na MOZET, kamisheni ya utalii Zanzibar na zingine.
Post a Comment