AFA KWA KUKOSA HEWA WAKATI AKISAFISHA KISIMA
Na Dinna Maningo, Tarime
MKAZI wa Kitongoji cha Lamboni Kijiji cha Nyangoto , Mrimi Werento amekufa wakati akisaficha kisima kilichopo nyumba ya kulala wageni ya Sunciro inayomilikiwa na Maiso Marwa Katika Kitongoji cha Kebhamonche Kijiji cha Mjini Kati Kata ya Matongo-Nyamongo wilayani Tarime mkoani Mara .
Wakizungumza na DIMA Online Emmanuel Joseph ameeleza" Tukio limetokea Julai, 8, 2023 saa tano asubuhi, alikuwa anaishi na mke wake ila watoto wake wapo kijijini.
"Marehemu anakadiliwa kuwa na miaka 33, alikuwa amepanga nyumbani kwetu, alienda kufanya kibarua cha kusafisha kisima" amesema.
Ameongeza " Chanzo cha kifo ni kuvuta hewa chafu, kisima hakikuwa na maji, watu walijaribu kuingia kumtoa lakini kila aliyeingia alishindwa kwa sababu ya kukosa hewa.
"Mwenye mji baada ya kuona kila anaeingia hewa inakuwa mbaya na kutoka ndani ya kisima akaomba msaada mgodini kitengo cha uokoaji na zima moto wakamtoa lakini tayari alikuwa ameshakufa" amesema Emmanuel.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mjini Kati, Josephat Elias Harun jirani na Kitongoji kulikotokea tukio hilo amesema;
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mjini Kati, Josephat Elias Harun jirani
"Nilipigiwa simu na mwananchi ili kutoa msaada baada ya huyu jamaa kushindwa kuokolewa na watu waliokuwa karibu yake.
"Nilimpigia simu Mwenyekiti wa Kijiji cha mjini kati Bageni Isack Paul aliwaita watu wa rescue wa mgodi wakafika wakamtoa lakini alikuwa ameshakufa" amesema Mwenyekiti.
Mwili wa Marehemu umehifadhiwa Kituo cha afya Nyangoto.
Post a Comment