KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE ARIDHISHWA NA MIRADI WILAYANI MASWA
Na Samwel Mwanga, Maswa
KIONGOZI wa mbio za mwenge jitaifa ,Abdalla Shaib Kaim ameridhishwa na miradi ya maendeleo wakati wa mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2023 huu katika halmashauri ya wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu.
Amesema miradi yote ipo vizuri ni mapungufu madogo madogo ambayo Wilaya itayafanyia kazi ili kuboresha zaidi.
Mwenge wa Uhuru umepitia jumla ya miradi 11 ikiwemo ya Mazingira, Afya, Elimu, Mradi wa uwezeshaji vijana kiuchumi,Kilimo,Utawala Bora, Lishe,Maji iliyogharimu zaidi cha ya Tsh. Bilioni 1.5 na kati ya hiyo mradi mmoja umewekwa jiwe la msingi, miradi minne imezinduliwa, miradi 3 imetembelewa na miradi 3 ilikaguliwa.
Akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa tenki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita Milioni moja, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Maswa,Mhandisi Nandi Mathias amesema kuwa moja ya faida za mradi huo ni kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji katika mji huo kutoka wastani wa masaa 12 kwa siku hadi wastani wa masaa 18 kwa siku.
Tenki la kuhifadhia Maji lenye uwezo wa lita Milioni Moja linalomilikiwa na Mauwasa ambalo limezinduliwa na Mwenge wa Uhuru Mwaka 2023
Amesema mradi huo umepunguza gharama za uendeshaji hususani gharama za umeme kwa wastani wa asilimia 20 kwa mwezi kutoka Tsh Milioni 30 kwa mwezi hadi Tsh Milioni 24.
Aidha Mhandisi Nandi ameishukuru serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuendelea kuipatia fedha mamlaka hiyo kwa ajili ya utekekezaji wa miradi mbalimbali ya Maji.
Naye Boniface Chatila ambaye ni Mwakilishi wa Kituo Cha Zana za Kilimo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) amesema kuwa kituo hicho kimeanzisha Kitovu cha Teknolojia za kihandisi (KITEK)katika kijiji Cha Mwandete wilaya ya Maswa kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya hiyo kutokana na kutoenea kwa kasi inayoridhisha ya matumizi ya zana sahihi za kihandisi hususan Zana za Kilimo na mifugo katika wilaya hiyo.
Moja ya zana za Kilimo zinazopatikana katika Kitovu cha Teknolojia za kihandisi(KITEKI) katika Kijiji Cha Mwandete wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu.
Amesema kuwa mpaka sasa Kitovu hicho kina jumla ya mashine mchanganyiko zipatazo 70 na baadhi yake zipo kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa wa Simiyu na Tabora zikiwa zinatumika kufanya kazi.
Aidha amesema kuwa huduma zinazotolewa na Kitovu hicho ni pamoja na ukodishaji na uuzaji wa mashine zikiwemo na mashine za kuongeza thamani ya mazao,kutoa mafunzo kwa wananchi juu ya matumizi sahihi ya mashine na Zana kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali katika sekta za Kilimo,mifugo na uvuvi na kuwa chanzo cha Upatikanaji wa mashine muhimu zinazotengezwa nchini na zinazoingizwa kutoka nje ya nchi.
Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu zilianza katika Wilaya ya Busega na kumalizia katika wilaya ya Maswa na kesho utakabidhiwa katika mkoa wa Shinyanga baada ya kumaliza kukimbizwa katika mkoa huu.
Bwawa la New Sola ambacho ndicho chanzo kikuu Cha Maji katika mji wa Maswa na Vijiji 12 katika wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu
Post a Comment