HEADER AD

HEADER AD

MATAPELI 11 WANAOTUMA UJUMBE ' TUMA KWA NAMBA HII' WADAKWA TANGA

>>Wakutwa wakiwa na line za simu zaidi ya 400 na vifaa mbalimbali vya mawasiliano

>>Wanatoka mikoa mbalimbali na wanaishi nyumba ya kupanga mkoani Tanga

Na Boniface Gideon, Tanga

MATAPELI 11 wanaojihusisha na kutuma ujumbe wa Simu maarufu ' PESA HIYO TUMA KWENYE NAMBA HII JINA ..' wamekamatwa na jeshi la Polisi mkoa wa Tanga mapema wiki hii wakiwa na laini za Simu zaidi ya 400 na Vifaa mbalimbali vya mawasiliano.

Katika orodha hiyo ya matapeli 11 wamo wanawake wawi '2' na waliobakia ni Wanaume ambapo wametambuliwa kwa majina ya Hadija Nyange '34'mkazi wa muheza, Zaina Athuman '25' Tanga Mjini, Innocent Omeme '35' mkazi wa Dar es Salaam, Abdul Aziz Nzori '31'mkazi wa Dar es Salaam.




Wengine ni Said Hassan '24'mkazi wa Dar es Salaam, Rashid Hassan '23' mkazi wa Dar es Salaam, Said Juma '30' Dar es Salaam,Idd Kaniki 35' Dar es Salaam, David Rupians 22' Dar es Salaam, Omary Mohamed '27' mkazi wa mkanyageni muheza na Salumu Salum '24' mkazi wa Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga Henry Mwaibambe amewaambia Waandishi wa Habari mapema Alhamis kuwa matapeli hao wametoka mikoa mbalimbali nchini na kuweka kambi kwenye moja ya nyumba ya kupanga iliyopo kata ya mnyanjani eneo la Donge ambapo wanalipa kodi ya Nyumba sh.800,000 kwa mwezi.




"


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga Henry

Wamepanga nyumba nzima na tumewakuta na vifaa mbalimbali ikiwamo majiko,laini za Simu,Simu aina mbalimbali pesa Tsh. Milioni 2,085,000 na karatasi ambazo zinakumbukumbu za majina ya Watu waliotapeliwa ambapo wanaweka alama ya vema 'tiki' kwa mtu aliyetapeliwa na laini husika huichoma moto" Amesema Mwaibambe.



No comments