HEADER AD

HEADER AD

NDEGE YA KIJESHI ILIYOKUWA IMEBEBA MARUBANI YAANGUKA ZIWA VICTORIA



Na Alodia Babara, Bukoba

NDEGE ya kijeshi iliyokuwa imebeba marubani wawili yenye namba JW 9127 imeanguka ziwa Victoria karibu na uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera wakati marubani hao wakiwa kwenye mazoezi.

Tukio hilo limetokea leo, Julai, 20, 2023saa 3:30 asubuhi ambapo ndege marubani hao wakiwa kwenye mazoezi ya kijeshi ndege yao ilidondoka ziwa Victoria karibu na uwanja wa ndege Bukoba.




Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Blasius Chatanda amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwataja marubani hao kuwa ni Leonard Nkundwa (45) na Alex Venance (30) ambao wamelazwa hospitali ya mkoa Bukoba kwa ajili ya uangalizi wa madaktaria 

Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo mkazi wa Nyamkazi Theophilda Kamaleki amesema toka jana jioni na leo asubuhi ndege mbili ndogo zilikuwa zinapita angani mara kadhaa sasa.

Amesema leo asubuhi wakati ndege hizo zikipita angani baadae ilianza kuonekana moja ndipo alipata taarifa ya ndege kudondoka kwenye maji huku majirani zake wakisema ni utayari wa majanga.


"Toka jana jioni ndege mbili zilikuwa zinapita angani mara kadhaa na leo asubuhi pia zilipita mara kadhaa zikiwa mbili zimeongozana baadae ilianza kuonekana ndege moja angani baadae nimepata taarifa kuwa moja imeanguka kwenye maji na wengine walikuwa wanasema ni utayari wa matukio lakini kumbe ilikuwa ni ajali.

Ni Takribani miezi tisa imepita toka ilipotokea ajali ya Precision Air na leo ndege ya Jeshi la Wananchi.



No comments