Home
/
TEKNOLOJIA/UBUNIFU
/
RC KINDAMBA : UWEKEZAJI KITUO CHA STEM PARK UTASAIDIA KUPATA WANASAYANSI MAHIRI
RC KINDAMBA : UWEKEZAJI KITUO CHA STEM PARK UTASAIDIA KUPATA WANASAYANSI MAHIRI
Na Boniface Gideon, Tanga
MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba ameonesha kufurahishwa na uwekezaji mkubwa wa Kituo Cha Sayansi mkoani Tanga Cha STEM PARK kilicho chini ya usimamizi wa Project Inspire kwakushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Tanga pamoja na Wadau wa Maendeleo.
Ni katika ziara yake ya kukagua miradi ya Tanga Yetu ambayo inasimamia miradi 17 katika Mkoa wa Tanga ikiwamo Ujenzi wa mradi wa Bustani ya kisasa ya mapumziko Jijini Tanga maarufu Forodhani,Kituo Cha Sayansi cha STEM PARK pamoja na mradi wa ugaji Kuku na ufugaji Majongoo Bahari.
Meneja wa Kituo Cha Sayansi mkoani Tanga Cha STEM PARK Max George ( kulia ) akitoa maelezo ya utendaji kazi wa Kituo hicho kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba Jana Wakati wa ziara yake ya kukagua Miradi ya Tanga Yetu ambayo inaendelea kutekerezwa na ambayo imekwisha malizika.
Kindamba amesema uwekezaji huo mkubwa wa Kituo cha Sayansi utausaidia mkoa wa Tanga kuzarisha Wanasayansi mahiri watakaokuja kulisaidia Taifa hapo baadae.
"Uwekezaji huu mkubwa wa Kituo cha Sayansi mkoani kwetu utatusaidia kupata wataalamu wengi hapo mbeleni na kiukweli nimefurahishwa sana na kitu kikubwa kama hiki kuwepo mkoani Tanga" amesema Kindamba.
Meneja wa Kituo Cha Sayansi mkoani Tanga Cha STEM PARK Max George ( mwenye Simu) akiwaonesha Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Tanga programu zilizobuniwa na Wanafunzi wa Kituo hicho na kuleta matokeo.
Amesema Serikali imeweka mazingira wezeshi ya elimu kwakuhakikisha kila mtoto anapata elimu bila vikwazo nakuwataka wazazi kuhakikisha wanawapatia watoto wao haki yao ya kupata elimu.
"Serikali imeweka Mazingira wezeshi ya Elimu, hivyo niwaombe Wazazi,walezi wahakikishe Watoto wanapata Elimu lakini pia wakitumie Kituo hiki ili tupate Wanasayansi mahiri wa baadae"Amesema Kindamba.
Post a Comment