VIKUNDI 40 KUSHIRIKI TAMASHA LA MUZIKI WA CIGOGO DODOMA
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dkt.Pindi Chana anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa tamasha la Muziki wa Cigogo ambalo mwaka huu ni la msimu wa 14, tukio litakalofanyika Julai 22, katika Kijiji cha Chamwino Ikulu, Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Sanaa Chamwino (CAC), Frank Mgimwa amesema mchakato wa maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vizuri na vikundi 40 vinatarajiwa kutoa burudani.
"CAC tumejiandaa vyema katika kukuza na kuendeleza utamaduni wa mtanzania kupitia Muziki wa Cigogo wa kabila la Wagogo ambapo mwaka huu kauli mbiu ni "Kuza Sanaa, Maadili kwanza".
Amesema vikundi vitawasilisha jumbe mbalimbali na kuonesha umahiri wao kupitia ngoma na nyimbo.
Vikundi hivi 40, kati ya hivyo 34 vinatoka Mkoa wa Dodoma na vingine 6 vinatoka nje ya Dodoma" amesema Frank Mgimwa.
Ameongeza kuwa vikundi hivyo sita vinatoka mikoa ya Iringa, Dar es Salaam, Singida na Zanzibar. Vingine ni pamoja na;
Kutoka Mkoa wa Dodoma ni kikundi cha Nyati, Swala, Nyota lamali, Nyerere, Ufunuo (Majeleko), Nuru, Nyundo, Ushirikiano, Jembe, Chibibi, Yeriko, Upendo, Nyemo, Ndagwa, Nyota njemana mengine mengi.
Post a Comment