LORENZ ARITHI MIKOBA YA YUSUF TAASISI YA BUSARA
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
TAASISI ya Busara Promotions inayoandaa tamasha la muziki la Kimataifa la Sauti za Busara visiwani Zanzibar, imemtambulisha Mkurugenzi mpya atakayesimamia taasisi hiyo.
Kupitia kwa Afisa Masoko na Meneja Mawasiliano wa Busara, ZakiaLulu amesema Busara wamemtambulisha rasmi Lorenz Hermann kuwa Mkurugenzi mpya akichukua nafasi ya Yusuf Mahmoud 'Dj Yusuf' umri 61 ambaye amestaafu nafasi hiyo aliyodumu kwa muda wa miaka 21.
"Busara imepata Mkurugenzi mpya, Lorenz Hermann ambaye ni mdau mkubwa wa Sanaa ya muziki wa kiafrika na kwingineko lakini pia amehudumu katika tasnia hii kwa zaidi ya miaka 5 akisimamia kazi za Sanaa na wasanii Zanzibar na Tanzania Bara
Kwa ujumla ni kiongozi sahihi ambae bila shaka atasimamia na kusongesha mbele taasisi na tamasha letu ." Amesema ZakiaLulu.
Pia Zakialulu amesema, Busara imepata Mtendaji mpya wa tamasha la Sauti za Busara, Journey Ramadhan amabaye kabla alikuwa meneja wa tamasha hilo.
Aidha, katika hatua nyingine Busara Promotions wapo katika hatua ya mwisho kupokea maombi ya wasanii wanaotaka kushiriki tamasha la 21 litakalofanyika Februali 9-11-2024, sambamba na kuendelea kuuza tiketi kupitia mtandao wao wa busaramusic (www.busaramusic.org).
Post a Comment