WANACHADEMA WAMPONGEZA RAIS SAMIA MRADI WA UJENZI MWISI SEKONDARI
Na Lubango Mleka,Igunga
WANANCHI wa Kata ya Mwisi Wilayani Igunga Mkoani Tabora, wameipongeza Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na wa Jamhuri ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia shule ya Sekondari ya Mwisi Tsh. Milioni 642 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa nane, mabweni matatu na matundu 12 ya vyoo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kijijini hapo wananchi hao waliojitambulisha kwa majina ya Cosmas Kalwisha, George Maige ambao ni wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Asha Hamis na kwandu Tungu, wamempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia fedha Kata hiyo.
Fedha hizo ni za ujenzi wa madarasa pamoja na kuendelea kutatua changamoto katika sekata ya elimu, afya na maji jambo ambalo limewapa matumaini na kuendelea kuiamini Serikali ya awamu ya sita.
" Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa mama yetu Samia kwa jitihada anazozifanya, nikizungumzia kata ya Mwisi kuna fedha zimetolewa kama Milioni 642, kazi inaendelea pale shuleni ya kujenga madarasa, mabweni na matundu ya vyoo.
"Kazi inafanyika nzuri sana kiasi kwamba hata ukifika wakandarasi na wanafanya kazi muda wote, diwani Jambeck na walimu wanasimamia kazi muda wote," amesema Kalwisaha.
George Maige amesema" Mimi ni Mwanachadema, katika miradi ya maendeleo ni lazima tuseme ukweli nikianzia katika Elimu, siku za nyuma tulikuwa tunachangishwa hela kila kaya lakini majengo yalikuwa hayaendi.
Kada wa CHADEMA,George Maige kushoto akipatiwa maelezo na diwani wa kata ya Mwisi Ahamed Jambeck, juu ya mradi wa ujenzi wa Madarasa, Mabweni na Vyoo katika shule ya Sekondari Mwisi.
"Katika utawala wa Rais Samia madarasa, mabweni yanaota kama uyoga, leo nimetembelea hapa shuleni nimeona kazi zinapigwa, kwa kweli inatia moyo sana, ili kuwa na maendele bora inaitaji kuwa na viongozi bora, Diwani anajitoa sana kufuatilia miradi yote hapa katani."
Aidha, Asha Hamisi na Kwandu Tungu, wamewataka wananchi wenzao, wanafunzi na walimu kusimamia miradi hiyo na kuitunza ili iweze kudumu kwa muda mrefu na kuhakikisha kuwa atakaye ihujumu basi anakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Ahamed Ibrahim Jambeck, amempongeza Mheshimiwa Rais Samia kwa kuwaamini watendaji wake katika ngazi ya chini na kuendelea kuwapatia fedha nyingi za miradi ikiwemo miradi ya afya, elimu, maji na umeme.
Bwalo la chakula na mikutano ambalo limegharimu kiasi cha Shilingi Milioni 100 likiwa limesima ujenzi wake kungojea fedha za awamu ya pili ilikuweza kukamilishwa ambalo limejengwa katika shule ya Sekondari Mwisi.
" Kwanza kabisa nitoe shukrani zangu kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutuamini viongozi wake katika ngazi za chini kwa usimamizi wa miradi. Fedha hizi tulizopewa zinafanya kazi ya ujenzi wa madarasa nane, mabweni matatu na matundu 12 ya vyoo.
" Waandishi wa habari nnajionea wenyewe jinsi kazi inavyo kwenda na kwa ubora unaotakiwa, pia tunatarajia majengo haya yote yakamilike kwa wakati uliopangwa," amesema Jambeck.
Ameongeza kuwa, mradi huo umetoa ajira za muda kwa zaidi ya wananchi 300 ambao ni mafundi, vibarua na wapishi, huku baadhi ya wafanyabishara wakinufaika na mradi huo kwa kuuza bidhaa kwa wafanyakazi, na vifaa vya ujenzi kwa mradi.
" Pia naishukuru Serikali ilitupatia Tsh Milioni 100, ambazo tumejenga bwalo kubwa la kisasa linalotumiwa na wanafunzi, nitoe tu rai kwa walimu, wazazi na wananchi kwa ujumla waendelee kuiamini Serikali yao.
Amewashauri viongozi kushirikiana kwa pamoja kuisimamia miradi kwa kufanya hivyo miradi itakuwa bora na kudumu kwa muda mrefu," amesema Jambeck.
Post a Comment