ACT- WAZALENDO TANGA WACHANGIA DAMU KUSAIDIA WAGONJWA
Na Boniface Gideon-Tanga
CHAMA cha ACT-WAZALENDO jimbo la Tanga pamoja na wakazi wa Jiji hilo wamejitokeza kuchangia Damu Salama kwaajili ya wagonjwa wanaopatiwa huduma kwenye Hospitali ya Rufani mkoa wa Tanga Bombo.
Uchangiaji huo wa Damu Salama umeenda sambamba na zoezi la uhamasishaji kwa jamii juu ya faida za uchangiaji wa Damu Salama ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani yanayofanyika kila Agosti 13 .
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa chama hicho mkoa wa Tanga, Rehema Mohammed amewaambia Waandishi wa Habari kuwa chama hicho kinatarajia kufanya kongamano la Vijana agosti 13 ikiwa ni kilele cha maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani hivyo katika kuelekea siku hiyo wameona ni vyema kuokoa maisha ya watu wengine.
‘’Kwakuzingatia umuhimu wa Damu hususani kwasisi wanawake chama chetu kimeona ni vyema kuokoa maisha ya watu wengine na tunaendelea kufanya hamasa hii kwa wakazi wote wa Tanga kujitokeza kwa wingi kwenye uchangiaji wa Damu’’ Alisema Rehema.
Sambamba na hayo Rehema amesema kabla ya maadhimisho hayo wanatarajia kufanya matukio mbalimbali ikiwamo mikutano ya hadhara na makongamano ya kuwaelimisha Vijana juu mambo mbalimbali ya nchi yao ikiwamo uzalendo kwa Taifa.
Kwaupande wake Katibu wa nNgome ya Vijana ACT-WAZALENDO jimbo la Tanga Kassimu Hassan aliwashukuru Wananchi kwakuitikia wito wakuchangia Damu.
Amewashukuru wakazi wa Jiji la Tanga kwa kujitokeza kwa wingi kuchangia Damu. Amewaomba waeendelee kuwa wazalendo kwa kuhamasishana kuchangia zaidi ili tuokoe maisha ya wengine lakini hata sisi pia ni wagonjwa watarajiwa’’ amesisitiza Kassimu.
Post a Comment