HEADER AD

HEADER AD

WATOTO WAWILI WANYONGWA, BABA NAYE AJINYONGA


Na Samwel Mwanga, Simiyu

WATOTO wawili ambao umri na majina yao hayajafahamika wamefariki kwa kunyongwa katika kijiji cha Mwantemi wilaya ya Itilima mkoa wa Simiyu.

Pia baba yao mzazi, Bundu Nghabi (32)Mkazi wa Kijiji Cha Kinamweli wilayani humo naye amekutwa amefariki kwa kujinyonga.

Akizungumza Leo na Waandishi wa habari,Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu,Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP),Edith Swebe amesema kuwa matukio hayo yametokea Agosti 11 mwaka huu majira ya saa 1:00 asubuhi.

    Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP),Edith Swebe

Kamanda Swebe amesema kuwa miili ya Watoto hao imekutwa imeninginizwa kwenye chumba wanacholala na Wazazi wao na uchunguzi unaonyesha dalili zote kuwa wamekufa kwa kunyongwa.

Pia amesema kuwa mwili wa baba Yao mzazi ulikutwa umeninginizwa juu ya mtu kwa kujinyonga.

Kamanda Swebe ameendelea kueleza kuwa Jeshi la Polisi katika mkoa huo linaendelea na uchunguzi wa matukio hayo huku likiendelea kumtafuta mke wa marehemu ambaye hadi sasa hajulikani mahali alipo.

Aidha Jeshi la Polisi mkoa wa Simiyu linatoa wito  kwa wananchi kutoa taarifa za migogoro ya kifamilia ili iweze kupatiwa ufumbuzi kwa kushirikiana na serikali za vijiji na Viongozi wa dini ili kujiepusha na matukio yasiyo ya kawaida.


No comments