HEADER AD

HEADER AD

PADRE ALIYEFARIKI KWA AJALI YA PIKIPIKI KUZIKWA AGOSTI, 21

Na Alodia Babara, Bukoba

 PADRE Asterius Mutegeki (33) mzaliwa wa kisiwa cha Bumbire wilaya ya Muleba mkoani Kagera aliyefariki kwa ajali ya pikipiki Agosti 18, 2023 anatarajiwa kuzikwa Agosti 21,2023.

Akizungumza Agosti 19,2023 Askofu msimamizi wa kitume wa jimbo Katoliki la Bukoba Methodius Kilaini amesema kuwa, Padre Asterius mazishi yake yanatarajiwa kufanyika Agosti 21,2023 katika makaburi ya mapadri Rubya Wilaya ya Muleba.

Askofu Kilaini amesikitishwa na kutokea kifo cha Padre huyo ambaye alipadilishwa Julai,2022, na hadi anakumbwa na umauti alikuwa anafanya kazi katika Parokia ya Ishozi wilaya ya Misennyi.

Amesema, Padre Asterius alikuwa mtoto wa kwanza katika familia yao, baba yake ni Wincheslaus Barongo diwani wa kata ya Bumbile wilaya ya Muleba na alikuwa Padre wa kwanza kutokea kisiwa hicho.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Blasius Chatanda amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa, bado alikuwa hajapata undani wa tukio hilo.

     Padre Asterius Mutegeki



No comments