RC SIMIYU AAHIDI MILIONI NNE BINGWA WA MICHUANO YA SIMIYU SUPER CUP
Na Samwel Mwanga, Simiyu
MKUU Wa Mkoa wa Simiyu, Dkt Yahaya Nawanda amesema kuwa bingwa wa Michuano ya soka ya Simiyu Super Cup 2023 anatarajia kubeba kitita cha Tsh. Milioni Nne.
Akizindua mashindano hayo na kuzungumza na viongozi wa vilabu ya soka na viongozi wa vyama vya soka vya wilaya zote za mkoa huo katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Simiyu Dkt. Yahaya amesema kuwa lengo la mashindano hayo ni kuwaunganisha vijana, kuleta umoja na mshikamano kwa vijana wa mkoa wa Simiyu kupitia mashindano ya Mpira wa miguu.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Dkt Yahaya Nawanda(mwenye kofia)akikabidhi Mpira mmoja wa wachezaji wa timu ambazo zitashiriki mashindano ya soka ya Simiyu Super Cup 2023
Amesema kuwa mashindano hayo yatachezwa kuanzia ngazi ya Wilaya na bingwa wa kila wilaya ataungana na timu nne kutoka wilaya ya Bariadi katika hatua ya robo fainali hadi fainali na michezo hiyo itafanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi na kwamba timu zitakazoshiriki ni 32.
Dkt Yahaya amesema kuwa atatoa jezi seti moja na mpira mmoja mmoja kwa kila timu itakayoshiriki hatua za awali za mashindano hayo pia na kwa timu zitakazoingia hatua ya robo fainali pia zitapewa tena seti moja ya jezi kwani anazo jezi za kutosha.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu mkoa wa Simiyu, Osuri Kosuri (kulia)akimpatia jezi Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Dkt Yahaya Nawanda jezi yenye jina lake wakati wa Uzinduzi wa Mashindano ya Simiyu Super Cup 2023.
"Mshindi wa kwanza kwenye mashindano haya atampata zawadi ya Tsh Milioni Nne, mshindi wa pili Milioni tatu na Mshindi wa tatu atampata Milioni Moja,"
"Tunagawa jezi seti Moja na Mpira mmoja kwa kila timu katika hatua hii ya Awali na hatua ya robo fainali pia tutatoa jezi seti Moja kwa kila timu kwa kuwa tunazo jezi za kutosha,"amesema.
Amesema kuwa mashindano hayo yataratibiwa na Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Simiyu(SIFA) huku akiwaagiza wakuu wa wilaya zote za mkoa huo kuwa walezi wa timu zinazoshitiki mashindano hayo kwenye wilaya zao.
Aidha amesema kauli mbinu ya Mashindano hayo itakuwa "Tumekiwasha,Tumekufikia, twende pamoja na Mama Samia".
Naye Mwenyekiti wa SIFA,Osuri Kosuri amesema kuwa kilichofanywa na Dkt Nawanda hakujawahi kutokea kufanywa na kiongozi yeyote wa serikali mkoani humo tangu uanzishwe na kuhakikisha kuwa watayasimamia kwa kufuata kanuni zote 17 za mchezo wa mpira wa miguu.
Post a Comment