HEADER AD

HEADER AD

RPC MARA ASEMA USHIRIKIANO WA POLISI NA WANANCHI UMESAIDIA WATUHUMIWA 100 KUKAMATWA

Na Jovina Massano, Musoma

MIEZI kadhaa iliyopita kuliibuka matukio mbalimbali ya uhalifu yakiwemo ya wizi na mauaji hali iliyopelekea wananchi wa mkoa wa Mara kuingiwa hofu na amani kutoweka.

Katika kuirejesha amani na usalama wa raia, Jeshi la Polisi mkoani humo likaendesha msako mkali kukabiliana na wahalifu ambao umezaa matunda na watuhumiwa kukamatwa.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mara Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Salim Morcase amewaambia Waandishi wa Habari kuwa, ushirikiano wa Jeshi la Polisi mkoani Mara na wadau wa ulinzi na usalama yakiwemo mashirika ya kijamii yasiyo ya kiserikali umesaidia kuimarisha usalama na amani katika mkoa.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mara Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Salim Morcase

Kamanda Salim amesema hayo Agost, 21, 2023 alipokuwa akitoa taarifa ya miezi miwili ya hali ya usalama ya mkoa ilivyo kwa Kipindi cha mwezi Julai na Agosti.

Amesema msako huo uliofanywa na Askari wa Jeshi la Polisi kwenye wilaya 4 umefanikisha kukamatwa watuhumiwa zaidi ya 100 wa makosa ya wizi,uwindaji haramu uuzaji wa madawa ya kulevya aina ya bangi,pombe haramu ya moshi (gongo),risasi na upatikanaji wa nyara za serikali.

Mafanikio haya yametokana na utoaji wa elimu kwa wananchi  katika mikutano ya hadhara inayoendelea kutolewa na Jeshi hilo katika maeneo mbalimbali.

"Mikutano tunayoifanya na vikao vya ana kwa ana kwa wananchi  imepelekea Jeshi la Polisi kuwa karibu nao na kutuwezesha kupata taarifa za waharifu na uharifu kwa haraka na kuzishughulikia kwa wakati", amesema Morcase.
 
Ameongeza kuwa katika mafanikio hayo yamesaidia kukamata risasi zipatazo 39 zinazotumika katika siraha aina ya Riffle na mtuhumiwa ameishafikishwa mahakamani, kilo 45.54 na kete 452 za bangi,Lita 1239 za pombe haramu ya moshi ( gongo)ikiwemo mitambo 4 ya kutengenezea pombe hiyo,nyaya 2 na rola za kutegea wanyamapori,vipande 56 vya nyamapori, wanyamapori 21 waliuwawa katika hifadhi ya Serengeti.

Mbali na hayo Jeshi hilo limefanikiwa kukamata mali zinazodhaniwa kuwa za wizi ni luninga 2 aina ya LG na pikipiki 21 za aina tofauti tofauti ambazo ni MC 945 BFR SANLG,MC 568 DLT Honda,MC 438 DSP KINGLION,MC 510 DVN Super tiger,MC 616 ATA Toyo,MC 828 CKB honda,MC  873 BFU honda.

Zingine ni MC 959 CHP Honda,MC 220 AGW Honda, MC 569 BYE Honda,MC 565 BYE,MC 145 CNH honda,MC 564 DNF KINGLION, MC 475 BWA Honda, MC 873 BFU honda, MC 621 CKJ Honda, MC 200 BZD TVS,MC 880 BTP Honda, MC 945 CMX TVS, MC 568 DLT Honda na pikipiki 1 haikuwa na namba za usajili.

Amesema kuna mali za wizi zilizoondolewa ambazo ni Luninga 1 aina ya LG,deki 2 aina ya LG na Sumsang ,kisemeo 1,Spika 2 nyeupe,Kamera 1 aina ya Canon, Ngamizi Pakatwa (laptop)6  aina ya ACER na Tarakilishi au Ngamizi (computer)1 aina ya Lenovo hivi vyote ni mali ya mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) Musoma.

Mwandishi wa DIMA Online amefanikiwa kuwahoji baadhi ya wananchi ambapo kwa upande wake Thereza Mkama mkazi wa Majitaroad amesema kuwa hivi sasa matukio ya wizi, uporaji na ukabaji yamepungua siyo kama kipindi cha nyuma hali haikuwa shwari.

                 Thereza Mkama

" Maeneo ninayoishi hivi sasa hali ni shwari Polisi waendelee na doria za mara kwa mara kuzidi kuleta amani kwa sisi wananchi na mali zetu"amesema Thereza.

Nae Victor  Ryangaro mkazi wa Kwangwa ameliomba Jeshi la Polisi liendeleze ushirikiano na wananchi ili hali ya usalama iendelee kuimarika.

               Victor  Ryangaro

"Kwa ujumla kwa sasa hali imetulia ni tofauti na miezi mitano iliyopita sasa hivi tunatembea kwa uhuru matendo ya kutekwa na wizi havisikiki kama hapo nyuma.

Amewaas wananchi kuendelea kutoa taarifa kwa wakati ili Jeshi liweze kudhibiti kwa haraka uharifu pindi unapotokea"amesema Victor.

Hata hivyo wamemuomba Kamanda wa Polisi mkoa kushiriki katika vikao vya Kata ili kuweza kuongeza imani kwa wananchi katika utoaji wa taarifa za waharifu katika maeneo yao.

           

No comments