HEADER AD

HEADER AD

DAS KALAGHE : WAKUU WA DIVISHENI HALMASHAURI YA MASWA SIMAMIENI AFUA ZA LISHE


 Na Samwel Mwanga, Maswa
 
WAKUU wa Divisheni na Vitengo katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa wanaotekeleza fua za lishe wametakiwa kusimamia utekekezaji wa masuala yote ya lishe ili kukabiliana na hali duni ya lishe katika jamii.

Hayo yameelezwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Athuman Kalaghe wakati akizungumza na wajumbe wa kamati ya lishe ya  Halmashauri hiyo katika kikao cha kutekeleza afua za lishe mwezi Januari hadi Machi na Mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu.

          Mkuu wa Divisheni ya Elimu Awali na Elimu Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa,Dkt Lucy Kulongwa(aliyesimama)akitoa taarifa ya utekekezaji wa Afya za Lishe katika Divisheni hiyo

Amesema kuwa suala la lishe ni agenda ya kitaifa na wilaya hiyo inalipa suala hilo umuhimu mkubwa ili kuondokana na tatizo la udumavu.

Divisheni na vitengo vyote vinavyohusika na utekekezaji wa afya za lishe zifanye majukumu hayo kwa ueledi wa hali ya juu.

"Wakuu wa divisheni na vitengo katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa msipofanya vizuri katika masuala ya Afua za lishe mtakuwa mmeiangusha wilaya yetu hivyo niwaombe suala hili mlipatie kipaumbele lengo letu tuondoke udumavu kwa Watoto wetu,"

"Binafsi sitaweza kuvumilia kwa Mkuu yeyote wa Divisheni au kitengo ambaye atashindwa kutekeleza majukumu yake ya Afua za lishe maana huyo atakuwa anatuangusha jambo ambalo sitaweza kulikubali,"amesema.

Amesema kuwa katika kusimamia jambo hilo ni lazima kwa kila Divisheni na vitengo kutengeneza Mpango kazi wa afua za lishe na kila juma apate taarifa za utekekezaji wa masuala yote ya lishe yalivyotekelezwa.

    Wajumbe wa Kamati ya Lishe katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu wakiwa katika kikao.

"Kila Mkuu wa divisheni na vitengo katika Halmashauri ya Wilaya yetu ya Maswa awe na mpango kazi kwa ajili ya utekekezaji masuala yote ya afua za lishe na kila juma nipate taarifa ya utekekezaji wake kwa hili ni lazima tulipe kipaumbele,"amesema.

Awali akitoa taarifa za utekekezaji wa afya za lishe kwenye Divisheni na Vitengo, Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi,Dkt Lucy Kulongwa amesema kuwa kwa sasa shule za ssingi katika wilaya hiyo zinatoa uji au chakula cha mchana kwa wanafunzi kwa asilimia 95.

"Katika kutekeleza suala la utoaji wa chakula cha mchana au uji kwa wanafunzi wa shule za msingi tumefanya vizuri hadi sasa tumefika asilimia 95 na kwa shule ambazo hazijaanza

" Tunaendelea na jitihada za kutoa elimu kwa wazazi na walezi wa wanafunzi ili waone umuhimu wa kutoa chakula shuleni ili waweze kuchangia chakula kwa watoto wao wawapo shuleni,"amesema.

Naye Mkuu wa Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Robert Urassa amesema kuwa wameendelea kugawa mbegu za viazi lishe kwa kila Kijiji na taasisi zote za serikali zikiwemo shule za msingi na shule za sekondari sambamba na kutoa elimu ya kilimo cha bustani jambo ambalo kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kutokana na kuwatumia maafisa ugani.

  Mkuu wa Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Robert Urassa (aliyesimama)katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu akisoma taarifa ya utekekezaji wa Afya za Lishe kwenye Divisheni hiyo.

Pia amesema kuwa wamekuwa wakihamasisha jamii suala la unywajji wa maziwa na hivi karibuni wameweza kutekeleza wiki ya maziwa kwa kutoa elimu ya unywajji wa maziwa kwa wanafunzi wa baadhi ya shule za msingi katika mji wa Maswa.

Kwa upande wake Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Abel Gyunda amesema kuwa, hali mbaya ya utapiamlo inasababishwa na ulishaji duni, maradhi ya mara kwa mara na huduma hafifu za malezi na makuzi ya awali ya watoto wadogo hivyo" amesema.

  Afisa Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Maswa,Abel Gyunda(aliyesimama)akitoa taarifa ya hali ya Lishe katika wilaya hiyo kwa wajumbe wa kamati ya Lishe ya Wilaya hiyo.

Ameongeza kuwa ni lazima kwa umoja wao wapambane kutokomeza hali hiyo kwa kutekeleza kikamilifu Afua za Lishe.

 “Utapiamlo unachangia maradhi, vifo na uchelewaji wa ukuaji wa mwili na maendeleo ya akili kwa watoto hivyo kwa umoja wetu tulifanya kazi na kila mmoja wetu akatekeleza wajibu wake kwenye masuala ya Afua za Lishe tutakabiliana na hali hiyo,"amesema.


No comments