SHIRIKA LAKABIDHI BOTI KWAAJILI YA ULINZI RASILIMALI BAHARI
Na Boniface Gideon, Mkinga
WAKAZI wa Vijiji 5 kati ya 9 vilivyopo Kata ya Boma wilayani Mkinga mkoani Tanga vimenufaika na Mradi wa utunzaji wa Rasilimali Bahari unasimamiwa na Shirika la Mwambao Coastal Community Network Tanzania Baada ya kukabidhiwa Boti kwaajili ya kuongeza Ulinzi Shirikishi kwa Jumuiya za Usimamizi wa Rasilimali Bahari za CFMA na BMU.
Boti hiyo imekabudhiwa Agosti, 26, 2023 yenye thamani ya Tsh Milioni 35 iliyotolewa kwa Vijiji vya Boma kichakamiba,Mwaboza,Boma Subutuni na kwamba itasaidia kulinda Rasilimali Bahari ikiwemo kuzuia uvuvi haramu.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Mwambao Coastal Community Network Tanzania Said Khalid (mwenye kipaza sauti) akikabidhi Boti ya Ulinzi Shirikishi kwa Jumuiya za Usimamizi wa Rasilimali Bahari kata ya Boma wilayani Mkinga mkoani Tanga leo.
Boti hiyo imekabidhiwa ikiwa ni miezi michache imepita Baada ya Wavuvi na wakazi wa Vijiji hivyo kupatiwa Elimu ya Ufugaji wa miamba Bahari ambayo imesaidia Wavuvi kuvuna Samaki Wengi aina ya pweza kila Baada ya siku 90 kwa kupitia njia ya ufungaji wa miamba Bahari.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika Hilo Said Khalid amesema Boti hiyo itawasaidia wakazi wa Vijiji kuongeza Ulinzi Shirikishi Baharini.
"Boti hii itasaidia kuongeza Ulinzi Shirikishi wa Rasilimali Bahari,lengo kubwa nikuhakikisha Rasilimali Bahari zinawainua Kiuchumi wakazi wa Vijiji hivi" amesema Khalid.
Khalid amesema wataendelea kutoa Elimu ya Mazingira kwa wakazi wa Vijiji kata hiyo.
"Shirika letu litaendelea kutoa msaada wa Vifaa kazi na Elimu ya Mazingira na tutaendelea kushirikiana na Serikali,wakazi wa Vijiji hivi katika kuhakikisha Bahari inawaletea manufaa wakazi wote hususani Wavuvi" Amesitiza Khalid.
Akipokea msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Surumbu amelishukuru Shirika Hilo kwa msaada huo nakuwataka Wadau mbalimbali kuendelea kuisaidia Jamii ya Mwambao wa Bahari ili Matumizi ya Bahari yaweze kuleta matokeo chanya ya Kiuchumi kwa wakazi.
Mkuu wa Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga Kanali Maulid Surumbu ( kulia) akikabidhi hati ya Mkataba wa Boti ya Ulinzi Shirikishi kwa Mwenyekiti wa Jumuiya za Usimamizi wa Rasilimali Bahari BMU Wilayani humo Kassimu Alfan,Boti hiyo imetolewa na Shirika la Mwambao Coastal Community Network Tanzania kwaajili ya kusaidia Ulinzi Shirikishi kwa Vijiji 5 vya kata ya Boma.
"'kwaniaba ya Wakazi wa Wilaya ya Mkinga tunatoa Shukrani Sana kwa msaada huu tunawaahidi kuwa msaada huu utatumika kama ilivyokusudiwa , niwaombe Wakazi wa Boma hususani Wavuvi nendeni mkaitumie Boti hii kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo " Amesema.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa Jumuiya za Usimamizi wa Rasilimali Bahari CFMA ( BMU) Wilaya ya Mkinga Kassimu Alfan ameshukiru msaada huo nakwamba awali kabla ya kupokea msaada huo walikuwa wanatumia mitimbwi na majahazi kufanya doria za Ulinzi Baharini Hali iliyowawia vigumu kuwapata wahalifu.
"Awali tulikuwa tunateseka sana kufanya Ulinzi Baharini kutokana na kukosa Vifaa vya kisasa kwakuwa wahalifu Wengi wa Baharini wanatumia Boti za kisasa hivyo ilikuwa ni vigumu kuwakamata kirahisi lakini kwasasa tutawakamata kwa urahisi kwakuwa tunavifaa vya kisasa zaidi".
Post a Comment