WAZIRI AWESO AZINDUA BODI 25 ZA MAMLAKA ZA MAJI NCHINI
Na Samwel Mwanga, Dar es Salaam
WENYEVITI wa Bodi za Mamlaka za Maji hapa nchini wametakiwa kuhakikisha wanazisimamia Mamlaka hizo ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi kwa kuhakikisha adhima ya Rais Dkt Samia Suluhu ya kumtua mama ndoo kichwani inatimia.
Hayo yameelezwa Septemba, 26,223 na Waziri wa Maji,Jumaa Awesome wakati wa uzinduzi wa Bodi 25 za Mamlaka za Maji Tanzania Bara sambamba na Mafunzo kwa wajumbe wa bodi hizo na Menejinenti zao uliofanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza Jijini Dar Es Salaam.
Waziri Aweso amesema kuwa bodi hizo zina majukumu mbalimbali lakini jukumu kubwa ni kuhakikisha zinasimamia Mamlaka zao ili ziweze kuwapatia Wananchi huduma ya Maji safi na salama katika maeneo yao wanayoyasimamia.
Amesema kuwa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)ya mwaka 2020 imeeleza kuwa ifikapo mwaka 2025 upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi katika maeneo ya mjini yafikie asilimia 95 na maeneo ya vijijini asilimia 85 hivyo ni lazima Wizara ya Maji ifikie malengo hayo kama yalivyopangwa.
"Katika kufikia malengo yaliyowekwa ya upatikanaji wa Maji katika Ilani ya CCM ya mwaka 2020 ni lazima Wenyeviti wa bodi mkazisimamie hizo Mamlaka zenu ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi kwa kutoa ushauri ambao utadaidia upatikanaji wa Maji safi na salama kwa wananchi,"amesema.
Pia ameiagiza bodi hizo kushirikiana na menejimenti, kuweka mikakati ya kupunguza kiasi cha upotevu wa maji kwani Maji hayo yanatibiwa kwa gharama kubwa huku akiwasisitiza lisiwe jambo la kawaida.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mauwasa,Mhandisi Nandi Mathias(wa kwanza kulia)akifuatilia kwa ukaribu mafunzo ya Wajumbe wa bodi za Maji hapa nchini kwenye ukumbi wa Ubungo,Plaza Jijini Dar Es Salaam"Upotevu wa maji lisiwe jambo la kawaida haya maji yanatibiwa kwa gharama kubwa hivyo taarifa ikitolewa kuwa kuna maji yanamwagika ni vizuri ifanyiwe kazi haraka hivyo niwaombe wataalamu wa Maji wakiwemo wenzetu wa chuo cha Maji watafute mwarobaoni wa tatizo hili,"amesema.
Aidha amesema kuwa ni vizuri malalamiko ya watumishi wa mamlaka na wateja wao yakasikilizwa kwa wakati ili kuondoka migogoro ambayo inaweza kusababisha kazi kutofanyika kwa ufanisi.
Waziri Aweso ametumia fursa hiyo kuwapongeza Wakurugenzi wa Mamlaka za maji kwa kusimamia vyema fedha wanazoletewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali kwenye maeneo yao.
Amesema kuwa Wizara ya Maji kwa siku za nyuma ilikuwa inafanya vibaya lakini kwa sasa inafanya vizuri kutokana na mabadiliko makubwa katika sekta ya maji yaliyofanywa na serikali kwa kuwapatia kiasi kikubwa cha fedha katika kutekeleza miradi ya maji hapa nchini.
Baadhi ya wenyeviti wa Mamlaka za Maji nchini wakisikiliza Waziri wa Maji,Junaa Aweso (hayupo pichani)kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza Jijini Dar Es SalaamAwali Mhandisi Alex Kaaya kutoka Wizara ya Maji akieleza majukumu ya Bodi za Mamlaka za maji nchini amesema kuwa zinatakiwa kufanya shughuli zao kwa kufuata miongozo iliyowekwa na kutoingiliana na menejinenti zao.
Amesema kila bodi ijipime utendaji wake wa kazi na wakumbuke wameteuliwa na Waziri wa maji na anaweza kutengua uteuzi wao iwapo watashindwa kutekeleza majukumu yao.
Baadhi ya Wajumbe wa Mamlaka za Maji hapa nchini wakati wa Uzinduzi wa Bodi 25 za Mamlaka ya Maji Jijini Dar Es Salaam"Wajumbe wote wa bodi mmeteuliwa na Waziri hivyo mnawajibika moja kwa moja kwake hivyo fanyeni kazi kwa uaminifu na uadilifu na mkishindwa aliyewateua atatengua uteuzi wenu hivyo tekelezeni majukumu yenu vizuri ili tumuunge mkono Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kuwapatia Wananchi huduma ya Maji safi na salama,"amesema.
Naye Mwenyekiti wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Maswa (Mauwasa)Paulina Ntagaye pamoja na kumshukuru Waziri Aweso kwa kumteua kushika wadhifa huo kwa kipindi kingine cha miaka mitatu amesema kuwa kwa mafunzo hayo yanayoyapata atahakikisha wanakwenda kuisimamia mamlaka hiyo.
Ameongeza kuwa atahakikisha huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama inaboreshwa kwa kuongeza mtandao wa upatikanaji wa Maji hayo.
Post a Comment