ASKOFU MASANJA AZINDUA NYUMBA YA UASKOFU AICT DAYOSISI YA PWANI
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
ASKOFU Mkuu wa kanisa la AICT Mussa Masanja Magwesela amezindua nyumba ya Uaskofu ya Askofu wa AICT Dayosisi ya Pwani.
Uzinduzi huo umefanyika tarehe 28 Octoba 2023 katika eneo la Kibada katika wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam.
Akitoa taarifa ya ujenzi wa nyumba hiyo ya Uaskofu, Mwenyekiti wa ujenzi wa Nyumba ya Uaskofu AICT Dayosisi ya Pwani Hoseah Ezekiel Kashimba amesema jumla ya shilingi milioni 345 zinatarajia kutumika kikamilisha ujenzi wa nyumba hiyo.
Kwa upande wake Askofu Mkuu AICT Mussa Magwesela ameipongeza hatua ya ujenzi wa nyumba ya Uaskofu na kuwashukuru kwa wote walioshiriki nataka hizo.
Amesema kama kanisa limepiga hatua katika upanuzi wa masafa ya radio ya kanisa (Inland Radio) na kuweza kuirejesha shule ya Bishop Kanoni Nkola kwa kulipa deni iliyokuwa inadaiwa na Benki.
Aidha Katibu wa AICT Dayosisi ya Pwani Samwel Mhangwa amewashukuru wote walioshiriki kuchangia gharama za ujenzi wa nyumba ya Uaskofu. Pia amewatunuku vyeti kwa kazi nzuri.
Hadi sasa Nyumba ya Uaskofu AICT Dayosisi ya Pwani imefikia asilimia tisini na tano ili kukamilika.
Post a Comment