RC MTANDA ASEMA MAWASILIANO, MAHUSIANO MAZURI YA VIONGOZI YATASAIDIA KUIJENGA MARA
Na Shomari Binda, Musoma
MKUU wa mkoa wa Mara Said Muhamed Mtanda amekumbusha kuwepo kwa mawasiliano na mahusiano ya karibu ya viongozi ili kujenga mkoa.
Kauli hiyo ameitoa kwenye kikao cha pamoja baina ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) mkoa wa Mara na watumishi wa serikali.
Amesema pasipokuwa na mawasiliano na mahusiano ya karibu utekelezaji wa masuala mbalimbali kwa malengo ya kuujenga mkoa hayataweza kufanikiwa.
Mtanda Mkuu wa mkoa wa Mara Said Mtanda akizungumza kwenye kikao cha pamoja kati ya viongozi wa CCM na watumishi wa serikali chama na serikali ni muhimu kuwa na mawasiliano na hilo hufanyika kupitia vikao na kuzungumza kwa pamoja.
Amesema mawasiliano ni kitu muhimu ili kuweza kutekeleza masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufatilia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao" Kama mimi na katibu hatuna mahusiano mambo ya chama hayawezi kwensa na ya serikali pia hayawezi kwenda.
" Yapo mawasiliano ya chama na serikali na mahusiano ya mtu na mtu kama viongozi ili mambo yaweze kwenda",amesema Rc Mtanda.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara Patrick Chandi amesema kikao hicho sio cha kunyoosheana vidole bali ni kujenga umoja na kuuinua mkoa.
Amesema mkoa wa Mara ni lazima uinuke kama ilivyo mikoa mingine na hilo litafanikiwa kwa kuwa wamoja na kukutana kwenye vikao.
Post a Comment