BASATA WAMPONGEZA MCHORAJI GADI KWA KUANZISHA STUDIO YA UCHORAJI YA KOKO'TEN
Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam
BARAZA la Sanaa nchini (BASATA) limetoa pongezi kwa mchoraji Gadi Ramadhani kwa kuanzisha studio mpya ya kisasa ya kazi za uchoraji ya Msanii iliyozinduliwa rasmi mapema mwishoni mwa wiki, mtaa wa Mkwepu Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa BASATADkt. Kedmon Mapana ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo la uzinduzi amesema kuwa tukio hilo linaingia katika historia kwa msanii kuwa na studio ya kazi zake za sanaa katika kukuza sanaa na kukuza kipato chake na Nchi.
Akizungumza,Dkt. Mapana amesema ni furaha kuona sekta ya Sanaa ikipiga hatua kubwa ya namna hii.
"BASATA tunayo furaha kubwa kuona maendeleo ya sanaa ya Tanzania yanazidi kusonga mbele, lakini yakichukuliwa kwa nguvu ya Watanzania wenyewe.
Maendeleo ya sanaa nchini, sisi kama BASATA kazi yetu ni kuweka mazingira wezeshi ili wadua wetu wa sanaa wafanye kazi vizuri katika mazingira mazuri kwa furaha na kwa faida iwe kwa mtu mmoja mmoja ama kwa taifa kwa ujumla." Amesema Dkt. Mapana.
Aidha, Dkt. Mapana ameongeza kuwa, wao kama wasimamizi na walezi hawataki kuona wanafungia kazi za wasanii nchini zaidi wakitaka wafikie malengo yao kama alivyofanya Gadi Ramadhani kupitia Koko'ten studio.
"Kwa sasa hii studio ni habari ya mjini, sisi sote ni mabalozi sasa na tuisemee tunapotoka hapa, Tunataka eneo hili wadau wanafika hapa kushuhudia kazi za uchoraji za wasanii wetu, ikiwemo kununua kazi zao kukuza kipato.
Hata sisi pale BASATA tunapokea wageni, hivyo tutaweza kuwaleta hapa kusaidia kazi za wasanii wetu, Lakini pia kama BASATA tunachangia Tsh Milioni Moja,kama mchango wetu ili kuwezesha kuendelea kukua kwa studio hii, nawashukuru sana na tuendelee kusapoti kazi za wasanii wetu". Alieleza Dkt Mapana.
Kwa upande wake Gadi Ramadhani ambaye ni msanii wa uchoraji na mwanzilishi wa studio hiyo akiwa ndiye mtendaji mkuu wa studio hiyo ya Koko'ten, amewashukuru wadau kwa kujitokeza kushuhudia tukio hilo ambapo amebainisha kuwa kila mmoja ana umuhimu wake mpaka kufikia hapo.
"Watu wengi wanafahamu nimeanza kuchora nikiwa mdogo sana. Nimetokea mbali takribani miaka 15 hadi 17 ya uchoraji wangu naimani mtoto anaweza kuzaliwa na kuwa mkubwa.
Nafasi ya uchoraji wangu, familia yangu, ndugu na jamaa, tumelia njaa pamoja na kuwa na furaha pamoja hadi kufikia hapa naamini ukaribu wenu, kimawazo ndo uliofanya mimi kufika hapa. Amesema.
"Naamini nikiwa sehemu tulivu, ndo kazi zangu zinakuwa sehemu salama katika nafasi yangu ya kuchora, maana picha kabla sijaitoa ili kuileta huko kwenu nahitaji utulivu hivyo studio yangu hii itaendelea nipa fursa ya kufanya vizuri.
Ukoo wangu wa Gadi, utakuwa mkubwa uendelee kama wa Tingatinga, Mzuguno ama wengine katika vizazi vya sanaa ya uchoraji." Amesema Gadi.
Aidha,amefafanua kuwa, kwenye kazi zake kuna taswira ya mwanamke, ambaye amebeba maana kubwa katika familia, hivyo amekuwa akichora mwanamke na Pweza ambaye anawakilisha Mwanaume.
"Leo nimekualika ili uone sehemu ninapofanyia kazi, nimeshafanyia kazi nyumbani, na sehemu mbalimbali. nimefanyia kazi sehemu mbalimbali na sasa nakukaribisha hapa.
Mtaa huu ni mtaa mkubwa wenye chimbuko la historia ya eneo hili. Ili jengo ni eneo la kihistoria hivyo ufunguaji wa hii studio itaendana na shughuli zangu.
"Nawashukuru sana BASATA, wao ni walezi wetu, wanasaidia ili gurudumu ili kufungua njia.
Katika tukio hilo kazi mpya mbalimbali za msanii mchoraji Gadi Ramadhani ambaye ameendelea kujenga jina lake ndani ya Tanzania na nje kwa aina ya uchoraji wake kwa kutumia mkaa, Pia katika tukio hilo, kazi za wasanii wengine ziliweza kufungua rasmi studio hiyo iliopo gorofa ya pili ya jengo la City House, mtaa wa Mkwepu.
Baadhi ya kazi za wasanii wengine waliounga mkono tukio hilo ni pamoja:Kija CM, Aman Abeid, Undareti Mtaki,Thobias Minzi na wengine wengi.
Post a Comment