HEADER AD

HEADER AD

DC HAULE AWAHIMIZA WANANCHI KUJITOKEZA UPIMAJI ARDHI ILI WAPATAE HATI

Na Shomari Binda, Musoma 

MKUU wa Wilaya ya Musoma Dk. Khalfan Haule amewataka wananchi  kuchangamkia zoezi  la upimaji wa ardhi na kupata hati za umiliki.

Kauli hiyo ameitoa akiwa Kata ya Nyakato Manispaa ya Musoma alipokuwa akigawa hati kwa wananchi 70 waliopimiwa viwanja vyao.

Amesema zoezi la upimaji viwanja linaendeshwa  na maafisa ardhi Manispaa ya Musoma na mkoa wa Mara.

Dc Haule amesema kuwa hati ina umuhimu mkubwa katika umiliki wa ardhi ambayo uwezesha kupata mikopo kutoka taasisi za kifedha.

    Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dk. Khalfan Haule aliyeshika maiki

Amesema mtu anapokuwa na hati na apotaka kuongeza mtaji kwenye biashara anaweza kufika kwenye taasisi za kifedha akaongezewa mtaji.

Mkuu huyo wa wilaya amesema wananchi wenye maeneo ya viwanja ambavyo havijapimwa wanaweza kufika ofisi za ardhi wakapewa utaratibu na kupimiwa viwanja vyao.

" Nichukue fursa hii kuwapongeza wananchi ambao leo mnapokea hati zenu za umiliki wa ardhi ambazo zitawasaidia kwenye masuala mbalimbali.

"Kwa wale wenye viwanja ambavyo havijapimwa ni vyema wakafika ofisi za ardhi wakapata utaratibu wa kupimiwa na hati hutolewa kwa muda mfupi", amesema Dc Haule.

Kwa upande wao wananchi waliopokea hati hizo wameishukiru serikali kwa kutoa hati kwa muda mfupi tofauti na zamani.

Wemesema kipindi cha nyuma hati ilikulazimu kusafiri hadi Mwanza kufuata hati na sasa wanazipata wakiwa Musoma.

No comments