HEADER AD

HEADER AD

DIWANI 'IGWE' AWAHUSIA WAHITIMU KUTOJIHUSISHA NA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA


Na Shomari Binda, Musoma

DIWANI wa  Kata  ya  Iringo  Juma  Iddy  Hamis  maarufu " Igwe"  amewataka  wahitimu  wa  kidato  cha nne  kutojihusisha  na  kujiingiza  kwenye  matumizi  ya  madawa  ya  kulevya.

Kauli hiyo ameitoa  wakati  wa  mahafali ya 18 ya kidato cha nne ya shule ya sekondari Iringo alipokuwa akimuwakilisha mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo.

        Diwani wa Kata ya Iringo Juma Iddy Hamisi  'Igwe'akizungumza kwenye mahafali ya 18 shule ya sekondari Iringo

Amesema  suala la matumizi ya madawa ya kulevya imekuwa tatizo kwa vijana hivyo ni muhimu kupewa angalizo mapema.

Diwani huyo amewaambia wahitimu hao kutokubali kushawishiwa kujiingiza kutumia madawa hayo ikiwemo bangi.

Amesema matumizi hayo yamekuwa yakiwafanya vijana kutoendelea masomo na hivyo kutotimiza ndoto zao.

" licha ya ujumbe niliowafikishia kwa niaba ya mbunge mheshimiwa Vedastus Mathayo nami niwaambie jambo moja la kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya.

" Msijaribu kujiingiza huko mbunge ameniagiza kuwasisitiza kuzingatia elimu nami naongezea msijiingize kwenye matumizi ya madawa ya kulevya',amesema.

Amesema mbunge yupo kwenye vikao na amemuagiza kumuwakilisha na yale ambayo yameelezwa kwenye risala atamfikishia kwaajili ya utekelezaji.

Kwa upande wa wahitimu hao wamesema watazingatia ujumbe waliopewa na kamwe hawatajiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kutokana na madhara yake.



No comments