HEADER AD

HEADER AD

KABASA FC YATINGA NUSU FAINALI ESTER BULAYA CUP 2023


Na Shomari Binda, Bunda

TIMU ya Kabasa FC imekuwa ya  kwanza  kutinga hatua ya nusu fainali  ya mashindano ya Ester Bulaya Cup yanayoendelea mjini Bunda.

Kabasa imetinga hatua hiyo kwa kuifunga timu ya Amani FC bao 2-1 katika mchezo mkali wa robo fainali ya kwanza uliofanyika uwanja wa sabasaba.

Wakizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo,mashabiki wa timu ya Kabasa FC wamesema Amani sio timu ya kuwasumbua.

Wamesema walijipanga mapema na lengo lao tangu mwanzo ni kufika fainali na kuchukua ubingwa wa mwaka huu.

Mmoja wa mashabiki wa timu hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Juma Hamis amesema wanasubili timu watakayokutana nayo hatua ya nusu fainali.

" Tulisema mapema Amani sio timu ya kutusumbua ilikuwa zamani na tumethibitisha hilo.

"Tunasubili mpinzani wa nusu fainali na tunaamini yoyote anayekuja tutampasua na kutinga hatua ya fainali" amesema Juma.

Kwa upande wao mashabiki wa timu ya Amani FC wamesema timu yao imecheza vizuri lakini wamekosa matokeo kwenye mchezo .

Robo fainali ya pili itachezwa oktoba 26 kati ya Bunda kids na Kung'ombe FC huku mashabiki wakiombwa kujitokeza uwanja wa Sabasaba kuona burudani.

No comments