HEADER AD

HEADER AD

WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO WARIDHISHWA NA MIRADI YA TASAF

Na Samwel Mwanga, Maswa

WAKUU wa  Divisheni na Vitengo katika halmashauri ya Wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu  wameridhika na miradi inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF)kupitia Miradi ya kupunguza umasikini TPRP IV-OPEC IV wilayani humo.

Wakitembelea miradi hiyo Oktoba 3 mwaka huu iliyoko katika Jimbo la Maswa Mashariki, amesema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano uliopo baina ya viongozi, wataalamu na wananchi.

Wamesema kuwa wameamua kufanya ziara hiyo maalum ya kukagua miradi ya Wananchi inayotekelezwa na TASAF kwa lengo la kuwajengea uelewa wa pamoja kwa wakuu hao.

     Nyumba ya Mganga katika Zahanati ya Mwabayanda M katika wilaya ya Maswa iliyojengwa na TASAF.

"Kufanya kazi kwa ushirikiano ndio kumepelekea miradi hii kukamilika kwa kiwango kikubwa na kwa ubora kama tulivyoiona wakati wa ziara yetu tulipoitembekea, "amesema  Mussa Mwita ambaye ni  Mwanasheria wa Halmashauri hiyo.

Wamesema kuwa wamejifunza kushirikiana kwa ukaribu zaidi kati ya  Serikali na wananchi ni jambo la muhimu lililosababisha kukamilishwa kwa miradi kwa wakati.

"Mie hapa nimejifunza jambo moja kubwa sana kuwa mafanikio haya ya kutekelezwa kwa miradi ya TASAF kwa wakati imetokana na ushirikiano wa karibu kati ya serikali na wananchi,"amesema Simeon Makuru ambaye ni Afisa Biashara wa halmashauri hiyo.

Aidha wamewashauri wataalamu kutoka TASAF katika halmashauri hiyo kuwa maeneo ya vijijini yanayofanya  kazi vizuri katika kutekeleza miradi yaongezewe fedha za miradi mingi zaidi ili iwe kama motisha kwa wengine kufanya vizuri zaidi.

    Ujenzi wa Bweni la Wasichana wapatao 80 katika shule ya Sekondari Budekwa wilaya ya Maswa lililojengwa na TASAF.

Pia wametoa wito kwa wananchi  kuendeleza kutunza miradi hiyo ili ilete manufaa zaidi kwao na vizazi vijavyo.

Naye Mwezeshaji wa TASAF, Issack Singu ambaye ni Afisa Mazingira wa Tasaf amesema kuwa miradi mingi imeibuliwa na wananchi wenyewe kwenye maeneo yao kutokana na changamoto wanazokuwa wanakutana nazo.

"Hii miradi yote tuliyoitembelea imeibuliwa na wananchi wenyewe kulingana na changamoto zilizokuwepo katika maeneo yao ndiyo maana unaona ushiriki wao ni mzuri kwenye miradi hiyo,"amesema.

Mratibu wa TASAF wilaya ya Maswa,Grace Tungaraza amesema kuwa katika utekekezaji wa miradi hiyo  ya TASAF kwa mwaka wa fedha 2021/2022 halmashauri hiyo ilipokea kiasi cha Sh. 1,020,721,737.87 kwa ajili ya kutekeleza miradi 15 ikiwemo ya uboreshaji wa Miundombinu 10,Kukuza uchumi kaya miradi  miwili  na Ajira za muda tatu.

    Madarasa mawili na Ofisi ya Walimu iliyojengwa na TASAF katika shule ya Msingi Mwawayi wilaya ya Maswa.
Ameongeza kuwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023,Mei 5 mwaka huu pia wamepokea Tsh 451,927,281 kwa ajili ya miradi mitano ya uboreshaji miundo mbinu ya Elimu na Afya.

Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Ujenzi wa Bweni la Wasichana 80 katika shule ya Sekondari Budekwa kwa gharama ya Tsh.Milioni 89.5,Ujenzi wa madarasa mawili.

Miradi mingine ni Ofisi ya Walimu na Matundu sita ya choo katika shule ya Msingi Mwawayi kwa gharama ya Tsh. Milioni 76.7 na Ujenzi wa nyumba ya Mganga katika Zahanati ya Mwabayanda M kwa gharama ya Tsh. Milioni 55.5.

    Wanafunzi wa shule ya Msingi Mwawayi katika wilaya ya Maswa wakiwa kwenye darasa lililojengwa na kuwekewa madawati kupitia mpango wa TASAF

Pia ujenzi wa madarasa mawili,Ofisi Moja ya Walimu na Matundu sita ya choo katika shule ya Msingi Mwafa kwa gharama ya Sh Milioni 70.1,Ujenzi wa zahanati Kijiji Cha Mwakidiga kwa gharama ya  Sh Milioni 103.8 na Ujenzi wa zahanati katika Kijiji cha Bushitala kwa gharama ya Sh Milioni 103.8

Ziara ya kukagua miradi ya TASAF kwa halmashauri ya Wilaya ya Maswa imefanywa kwa lengo la kujengeana uelewa wa pamoja Wakuu wa Divisheni na Vitengo kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo kwa ngazi ya halmashauri.


      Mwalimu Alponary Mwinyi wa shule ya Sekondari Budekwa wilayani Maswa(aliye kati)akiwaelezea Wakuu wa Divisheni na Vitengo katika halmashauri ya Wilaya hiyo faida za Bweni la Wasichana lililojengwa na TASAF.

No comments