RC MTANDA ATOA MAAGIZO MAREKEBISHO UWANJA WA KARUME
Na Shomari Binda, Musoma
MKUU wa mkoa wa Mara Said Muhamed Mtanda ametoa wiki 2 uwanja wa kumbukumbu ya Karume ulekebishwe mapungufu yake na kuendelea kutumika.
Maagizo hayo yametolewa kwa wasimamizi wa shughuli za michezo manispaa ya Musoma na mkoa wa Mara kwa kushirikiana na wadau wengine.
Maelekezo na maagizo yamewagusa pia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira ( MUWASA) ambao pia wameagizwa kukaa kwa pamoja ili uwanja huo pia uweze kumwagiliwa eneo la kuchezea.
Akizungumza mara baada ya kuutembelea uwanja huo amesema kila mmoja atimize majukumu yake na uwanja huo utumike kwa michezo.
Mkuu wa mkoa wa Mara Said Muhamed MtandaAmesema timu ya Bunda Queen inayojiandaa na ushiriki wa ligi kuu ya wanawake na timu ya Biashara United inayoshiriki ligi ya Championship wanapaswa kuutumia uwanja huo.
Rc Mtanda amesema ndani ya wiki 2 anataka kuona marekebisho yote yamefanywa na kuahidi kuchangia sehemu ya marekebisho hayo.
" Nawaagiza mwende mkakae muone mnaanzia wapi kutekeleza yote niliyoyaagiza na ndani ya wiki 2 yawe yametekelezwa.
' Kila mmoja atimize majukumu yake na afisa michezo wa mkoa simamia maagizo haya na sio kila jambo kumsubili mkuu wa mkoa",amesema Rc Mtanda.
Mkuu huyo wa mkoa ameongeza kuwa haiwezekani wananchi wakose sehemu ya burudani kwa watu kushindwa kusimamia majukumu yao
Hivi karibuni bodi ya ligi inayosimamia ligi hapa nchini iliufungia uwanja wa Karume Musoma ili ulekebishwe ambapo baadhi ya maeneo yamesharekebishwa.
Post a Comment