WANAFUNZI 87,470 WANATARAJIWA KUFANYA MTIHANI WA DARASA LA NNE
Na Shomari Binda, Musoma
JUMLA ya wanafunzi 87,470 kutoka Mkoa wa Mara wanatarajiwa kufanya mtihani wa upimaji wa Kitaifa wa darasa la NNe (SFNA-2023) unatoratajiwa kuanza kesho tarehe 25 -26 Oktoba, 2023 hapa nchini.
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya elimu na ufundi Makwasa Bulenga imeeleza kuwa kati ya wanafunzi wote wanaotarajiwa kufanya mtihani huo, wasichana ni 43,341 na wavulana ni 44,129.
Mwalimu Bulenga ameeleza kuwa wanafunzi hao wanategemea kufanya mtihani katika jumla ya Shule za Msingi 905 zilizosajiriwa kufanya mtihani wa darasa la nne 2023 zilizopo katika halmashauri zote tisa za mkoa wa Mara.
Taarifa hiyo imeonyesha kuwa halmashauri ya Wilaya ya Tarime (141), Halmashauri ya Wilaya ya Rorya (140), Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti (130), Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (117) na Halmashauri ya Wilaya ya Bunda (110).
Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Butiama (94), Halmashauri ya Mji wa Bunda (72) Halmashauri ya Manispaa ya Musoma (59) na Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (42).
Taarifa hiyo imeonyesha kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime ina wanafunzi 15,767 Halmashauri ya Wilaya ya Rorya 12,957, Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti 11,927, Halmashauri ya Wilaya ya Butiama 10,080 na Halmashauri ya Wilaya ya Bunda 10,047.
Halmashauri ya Wilaya ya Musoma na Halmashauri ya Wilaya ya Bunda zina wanafunzi 8,144 kila moja, Manispaa ya Musoma 5,339, Halmashauri ya Mji wa Tarime 5,065.
Maandalizi kwa ajili ya kuanza mtihani huo yamekamilika na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara inawahimiza wazazi wote wenye watoto waliosajiriwa kuhakikisha wanafanya mtihani huo na inawatakia wanafunzi wote watakaofanya mtihani mafanikio mema.
Post a Comment