HEADER AD

HEADER AD

SERIKALI YATAKIWA KUTAMBUA MCHANGO WA WAANDISHI WA HABARI


Na Helena Magabe, Tarime

SERIKALI imetakiwa kuendelea kuthamini mchango wa Waandishi wa Habari kwa kuviondolea vikwazo vyombo vya habari na Waandishi wa habari.

Kauli hiyo imetolewa Joyce Sokombi  aliyewahi kuwa mbunge wa Viti maalumu ambaye pia ni mlezi wa Chama cha Waandishi wa habari Wanawake wenye  maono mkoa wa Mara (Visionary Womes Journalist), wakati wa uzinduzi wa chombo cha habari cha mtandaoni cha DIMA ONLINE BLOG.

                            Joyce Sokombi 

Sokombi amesema kuwa Waandishi wa habari wana kazi kubwa ya kufikisha taarifa kwa Jamii lakini bado mchango wao haujathaminiwa.

Aidha amesema ni vema Serikali ikatambua mchango wa Waandishi na kuondoa vikwazo vinavyokwamisha ufikishaji taarifa ili Wadau na Wananchi wapate taarifa.

Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo ambaye ni Mjasiriamali Bhoke Bwiso amempongeza mmiliki wa DIMA ONLINE, Dinna Stephano Maningo kwa hatua kubwa yakufungua blogu.

Bhoke Bwiso katika kuunga juhudi za waandishi wa Habari katika kuhabarisha umma, ameichangia ofisi ya DIMA ONLINE Tsh. Milioni moja (1,000,000) kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya ofisi 

Naye Emiliana Julius Range Rafiki wa karibu wa Dinna Maningo amemtia moyo na kumpongeza kwa hatua kubwa ya kumiliki Blogu ambaye amewahi kupata tuzo ya uandishi wa habari za uchunguzi huku akiahidi kununua Kamera yenye thamani ya Tsh. Milioni 2.5.

       Aliyesimama ni Emiliana Julius Range mkazi wa Nyamongo katikati ni Dinna Maningo Mmiliki wa DIMA ONLINE,na kushoto ni Rose Joseph Kimaro Mkurugenzi Mtendaji wa DIMA ONLINE 

Dinna Maningo katika mchakato wake wa kuanzisha blogu hiyo alianza kutoa habari zake kupitia  mtandao wa Instagram na Twitter.

Kufikia Septemba 21,2022 alisajili blog yake Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ( TCRA) na kikabidhiwa Leseni ya uendeshaji wa maudhui mtandaoni na hivyo kuanza kuripoti habari kupitia Tovuti ya www.dimaonline.co.tz zinazoripotiwa na Waandishi toka Mikoa mbalimbali.

Wadau mbali mbali kutoka sekta binafsi ,Viongozi wa Dini, Vyama vya Siasa, Wachimbaji madini, Makapuni, Ndugu na jamaa,Marafiki pamoja na Waandishi wa Habari wamejitokeza kumuunga mkono.

Katika uzinduzi huo washiriki wote kwa pamoja walichangia harambe kwaajili ya ununuzi wa vitendea kazi na kufikisha shilingi Milioni 10 pamoja na ahadi ya zaidi ya Milioni  20.

Mafanikio ya blogu hiyo tangu kuanzishi Septemba 21,2022 hadi kufikia Septemba 20,2023 Dima online imefanikiwa kuposti habari na makala mbali mbali na kufikisha jumla ya habari 566.


Kwa mujibu wa Dinna Maningo amesema malengo yake ni kuanzisha Tv online (YouTube) baada ya uzinduzi wa blog na kwa matamanio yake ya mbeleni ni kuja kuanzisha kituo cha Redio  pamoja na Runinga.

Aidha Maningo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa DIMA ONLINE, Rose Joseph Kimaro wamewashukuru watu wote walioshiriki katika uzinduzi huo wakiwemo wadau mbali mbali pamoja na Waandishi wa habari kwa kuitikia mwaliko wa kushiriki na kutoa michango yao. 



No comments