POLISI TARIME/RORYA WAIOMBA SERIKALI MILIONI 149 UNUNUZI SAMANI ZA OFISI
Na Helena Magabe, Tarime
JESHI la Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya limeiomba Serikali kutoa fedha Tsh. 149,500,000 kwaajili ya ununuzi wa Samani za ofisi, Ofisi kuwa na mfumo wa Tehama, pamoja na mfumo wa kuboresha ulinzi na Usalama.
Ombi hilo limetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Polisi Tarime, Rorya Kamishna Msaidizi wa Polisi Mark Njera wakati wa kusomwa Risala kwa Waziri wa mambo ya ndani Mhandisi Hamad Masauni alipokuwa akikagua mradi wa jengo la Ofisi ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Tarime/Rorya.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Polisi Tarime, Rorya Kamishna Msaidizi wa Polisi Mark Njera.
Masauni amekagua mradi wa jengo hilo la Polisi Tarime/Rorya ambalo ujenzi wake umegharimu Tsh. 1,564,953,000 ambao umekamilika kwa kupitia mfumo wa Force account.
Force account ni aina ya uendeshaji wa miradi ya ujenzi ambapo Taasisi za umma/ Serikali (Procurement Entity {PE}) au idara zinazohusika hutumia wafanyakazi na vifaa vyake au wafanyakazi walioajiriwa kwenye taasisi hiyo kuendesha na kusimamia
Kwa mujibu wa RPC Njera Mradi huo umekamilika kwa asilimia 100, ila hauna samani za ndani pamoja na ukuta.
Jengo la Ofisi ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya
Mradi wa jengo hilo ulianza Oktoba 23, 2021, katika ujenzi huo Jeshi la Polisi lilikumbana na changamoto nyingi katika utekelezaji wa mradi huo.
Imeelezwa kuwa changamoto hizo ni pamoja na kupanda kwa gharama za vifaa vya ujenzi,umeme kukatika mara kwa mara ambapo Jeshi hilo lililazimika kutumia jenereta ili ujenzi uendelee.
Aidha wataalamu wa Jeshi la zima moto na uokowaji wameshauri jengo hilo liwe na kuwepo mfumo wa dharula inapotokea kung'amua moto( automatic fire detection system), miundombinu maalumu ya watu kuweza kujiokoa na kuokolewa wakati wa dharula (emergency evocation plan).
Vingine ni mwanga wa dharula(emergency lighting system) alama za kuelekeza njia ya kutokea nje ya jengo wakati wa dharula (emergency exit signs) pamoja na milango na madirisha (emergency exit doors/windows.
Ujenzi wa ukuta wa kulizunguka jengo hilo ni mita za mraba( square meter 3.645).
Waziri Masauni alisema amepokea changamoto hizo na kuahidi kuwa Serikali itazifanyia kazi.
Post a Comment