TAASISI YA TYAIDNP NA HARAKATI ZA KUWAKOMBOA VIJANA KATIKA KILIMO CHA UMWAGILIAJI BUGWEMA
Na Dinna Maningo, Mara
WAHENGA wanasema kwamba Vijana ni nguvu kazi ya Taifa, wakiwezeshwa katika kilimo watajikomboa kiuchumi kwani jembe halimtupi mkulima na Kilimo ni uti wa mgongo.
Ibara ya 35 ya Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025 inasema kilimo cha kisasa ndio msingi katika kujenga uchumi, na kina nafasi ya kimkakati katika kukuza ustawi wa Taifa, mchango wa sekta ya Kilimo katika pato la Taifa ni wastani wa asilimia 65 ya Watanzania.
Ibara ya 37 ya Ilani hiyo ya uchaguzi inasema katika kipindi cha miaka mitano 2020-2025, Chama cha Mapinduzi (CCM) kitaendelea kusimamia Mapinduzi ya Kilimo ili kuhakikisha kinaendelea kuwa chenye tija na kinachotumia teknolojia ya kisasa.
A. Kusimamia kikamilifu hifadhi na matumizi endelevu ya maji, ardhi ya kilimo na mazingira sambamba na kuongeza miundombinu ya umwagiliaji itakayoendeshwa kiuchumi kwa kufanya yafuatayo;
(a) Kuongeza eneo lenye miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji katika hekta 56,383 mpaka kufikia hekta 1,200,000 ifikapo 2025. (1) Kuongeza eneo la umwagiliaji kwa hekta 111, 192 kwa kukamilisha ujenzi wa skimu za umwagiliaji 261 katika Mikoa 25.
Ilani hiyo inaeleza kuwa kati ya hizo skimu ndogo ni 179, skimu za kati 63 na skimu kubwa 19. Kujenga skimu mpya za umwagiliaji 208 nchini, kati ya hizo ndogo ni 123, skimu za kati 63 na skimu kubwa 22.
Ujenzi huo unatarajia kuongeza eneo la umwagiliaji kwa hekta 136, 928. Aidha, sekta binafsi itahamasishwa kushiriki kwenye ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji itakayoongeza eneo la umwagiliaji kwa eka 150, 000.
Pia kujenga na kuimarisha mabwawa ya uvunaji wa maji ya mvua 88 katika skimu za umwagiliaji kwa ajili ya kilimo cha mpunga na mazao mengine katika Mikoa 25 ili kuongeza maeneo ya kilimo cha umwagiliaji.
Kurejesha skimu ya umwagiliaji hekta 60,000 kwa kutumia fursa ya bwawa la Nyerere. Kuimarisha uendeshaji, usimamizi na matengenezo ya miundombinu ya umwagiliaji kwa uanzishaji na uendelezaji wa ushirika wa wanufaikaji wa umwagiliaji.
Katika Ilani hiyo imeelezwa kuanzisha mfuko wa umwagiliaji wa Taifa kwa ajili ya kukusanya mapato kutoka katika miradi ya uwekezaji wa umma ili kuendeleza na kufanya upanuzi wa miradi mipya ya umwagiliaji nchini.
Kuendelezwa na kuendeshwa kwa miradi ya umwagiliaji ya umma kibiashara kwa kuwashirikisha wakulima na wanufaikaji ili kupata mitaji ya upanuzi wa kilimo cha umwagiliaji nchini.
Kujenga mabwawa ya kuhifadhi maji kwa ajili ya umwagiliaji katika maeneo yanayopata mvua chache kama Kanda ya kati , Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kaskazini pamoja na maeneo yanayopata mafuruko ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuzuia mafuriko na kupanua kilimo cha umwagiliaji.
Pia kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza katika kilimo cha kisasa cha biashara hususani ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji na kuwashirikisha wakulima.
Utekelezaji wa Ilani
Katika kuhakikisha Vijana wanakuwa kiuchumi kupitia kilimo cha umwagiliaji, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imetoa ardhi katika Kijiji cha Bugwema ekali 500 na kuikabidhi Taasisi ya Mpango wa Mtandao wa Maendeleo ya Kilimo cha Umwagiliaji wa Vijana Tanzania (Tanzania Youth Agro Irrigation Development Network Programme) mkoani Mara.
Lengo ni kuiwezesha Taasisi kuwakusanya Vijana watakaowekeza katika kilimo cha umwagiliaji ili kujipatia kipato na kujiajiri na kujiinua kiuchumi badala ya kuwa tegemezi.
Taasisi ya Tanzania Youth Agro Irrigation Development Network Programme (TYAIDNP) ni kikundi chenye usajili Na. 18998 kilichoanzishwa mwezi 9 mwaka 2013.
Anna Frank Khamis ni Katibu wa Taasisi hiyo Mkoa wa Mara, anasema kuwa Taasisi hiyo ilianzia mkoani Kigoma mwaka 2013 na kupata mafanikio makubwa katika sekta ya kilimo na kutoa ajira kwa vijana wengi.
Anasema kuwa mafanikio ya Tanzania Youth Agro Irrigation Development Network Programme ndio chimbuko la kuona umuhimu wa kuzindua Taasisi mikoa mingine ikiwemo Mara iliyozinduliwa Septemba, 16, 2023 katika ukumbi ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mara.
"Tumeona ni vyema tuwahamasishe Vijana wenzetu kila wilaya kwa makundi mbalimbali ya jamii ili kuwa na nguvu ya pamoja katika kutekeleza malengo yetu kama Vijana na Taifa kwa ujumla katika utekelezaji wa sera ya kilimo kwanza na vitendo" anasema Anna.
Katibu huyo anasema kuwa TYAIDNP imeundwa kwa kuzingatia malengo ambayo jamii hasa vijana wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa ajira pamoja na ukosefu wa chakula katika Taifa na Afrika kwa ujumla.
Anna anasema kuwa Kilimo ni Sayansi inayohusika na shughuli za kilimo ili kuzalisha mazao kupata chakula kwa ajili ya matumizi ya binadamu na wanyama katika maeneo mengi hapa nchini.
" Sera ya Taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2017 imeweka wazi dira ya Serikali ya kuandaa mazingira wezeshi kwa vijana kushiriki kikamilifu katika shughuli zote za kijamii, kisiasa na kiuchumi ili kijikwamua kimaisha na kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana wengi na utegemezi katika jamii.
" Kwa kuthamini na kuunga jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu katika hotuba yake ya Septemba, 7, 2023 kwenye mkutano wa jukwaa la mifumo ya chakula Afrika 2023 ( AGRF) alisema kwamba;
Tanzania imejidhatiti kuingia katika masoko ya kikanda na kimataifa ili kukidhi mahitaji ya chakula katika nchi mbalimbali kwani nchi inayo fursa ya kuwa mzalishaji na msafirishaji mkubwa wa mazao ya chakula na biashara.
Katibu huyo anasema Taasisi kwakutambua umuhimu wa sekta hii ambayo ni uti wa mgongo wa Taifa, inajitahidi kuwaelimisha na kuhamasisha na kuwaunganisha vijana waweze kujiajiri kupitia fursa ya kilimo na ufugaji kwani ndio kundi kubwa linalokabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa ajira.
Anna anasema kuwa Taasisi hiyo imefanikiwa kupata ekari 500 kutoka Serikalini kwa ajili ya kilimo katika Kijiji cha Bugwema Kata ya Bugwema wilaya ya Musoma.
Changamoto za TYAIDNP Mara
Anasema Taasisi inakabiliwa na upungufu wa maeneo ya shughuli za kilimo na ufugaji kwenye baadhi ya Wilaya hivyo kupelekea Wilaya nyingine kuwa nyuma katika kutekeleza jitihada za Rais kwenye sekta ya Kilimo.
Changamoto nyingine ni upungufu wa pembe jeo na zana nyingine za kilimo cha umwagiliaji kama vile Sola panel 12 Tsh.12,700,000, Sim tank 3pcs Tsh. 3,900,000, Mota 3pcs 2,100,000, Pipe za umwagiliaji 3 Pcs 3,000,000, Tofari 600 tsh.600,000.
Pia Saruji 6bgs 150,000, Nondo 3pcs 69,000, Wire mesh 3pcs 60,000, Biding wire 3pcs 8,000, mbao 10 Pcs 140,000, mahema 5pcs Tsha 1,250,000, vitu vya shambani 100 pea 1,500,000. Jumla ya vifaa vyote ni 24,157,000.
Paul Joseph ni Katibu wa Taasisi ya Tanzania Youth Agro Irrigation Development Network Programme Wilaya ya Musoma, anasema kwa upande wa Musoma wamefanikiwa kupata eneo la ekari 500 ambazo zipo katika shamba la Bugwema.
Anasema wapo kwenye mchakato wa kuongezewa eneo baada ya Baraza la Madiwani kuridhia kuongeza eneo hadi kufikia ekari 2500 ambazo zitatumika kwaajili ya uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.
" Kinachosubiriwa ni fedha zitakazoendesha shughuli za kilimo. Mkakati wetu ili kufikia malengo ni kutafuta wafadhili watakaowekeza na kuwezesha shughuli za kilimo ili kufikia malengo yetu, kwani Taasisi bado haina pesa za kutosha kuwezesha shughuli za kilimo.
Anasema mwitikio wa vijana ni mkubwa sana kutokana na Vijana kuwa mtaani bila ajira hivyo wengi wamehamasika kujiunga na Taasisi kwaajili ya kufanya shughuli za uzalishaji kupitia kilimo ambayo ni fursa pekee iliowafikia.
Anna Frank anaishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Vijijini kwa kutoa eneo ekari 500 kwa ajili ya mradi wa vijana wa kilimo.
"Tunawashukuru viongozi wa Halmashauri ya Butiama, Bunda, Serengeti, na Rorya kwa ushirikiano wao mzuri tuliopewa katika ufuatiliaji wa maeneo ya shughuli za kilimo.
" Pia napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru Serikali na uongozi wa mkoa kwa kutupatia ukumbi kwa ajili ya kongamano na wote waliochangia ili kufanikisha ambao ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama na wengineo " anasema Anna.
Uongozi wa Taasisi hiyo unawapongeza vijana waliokubali kujiunga na na Taasisi kwani ni mwanzo mzuri wa kuingia kwenye uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara katika mkoa wa Mara na kuinua uchumi wa vijana na mkoa kwa ujumla.
Msisitizo wa sheria ya umwagiliaji
Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji Na 4 ya mwaka 2013 iliyotungwa na kupitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2013, na kutiwa saini na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tarehe 20/10/2013.
Lengo la kutungwa kwa sheria hiyo ni Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kusimamia kilimo cha umwagiliaji nchini. Sheria hiyo ilitungwa ili kuondoa changamoto zilizokuwa zinaikabili sekta ya umwagiliaji.
Changamoto hizi ni pamoja na ushiriki mdogo wa wakulima na sekta binafsi katika ujenzi, usimamizi na uendeshaji wa skimu za umwagiliaji ambao hujengwa na Serikali kwa fedha nyingi.
Udhaifu wa mfumo wa kitaasisi ambao ulikuwa haukidhi kasi ya kuendelea kupanuka kwa nahitaji ya kilimo cha umwagiliaji kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu wengi na kupungua kwa mvua, hivyo kufanya watu wengi kujiunga kwenye kilimo cha umwagiliaji.
Uvamizi wa maeneo yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji. Sheria hiyo kifungu cha 45 (1) kinabainisha kuwa itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kufanya yafuatayo;
Kulima au kuingia katika ardhi ya umwagiliaji kwa madhumuni mengine zaidi ya kilimo cha umwagiliaji. Kuruhusi sumu ya viwandani au uchafu wa nyumbani katika skimu yoyote ya umwagiliaji, bila kutibu majikikamilifu.
Kuzuia ufanisi wa mambo mbalimbali ya mfumo wa matupio na kuhatarisha usalama wa mifereji ya kusafirisha maji ya umwagiliaji na matupio.
Kufungua au kufunga mlango au chombo cha kudhibiti mwenendo wa mafuriko kwenye bwana, mifereji au mfumo wowote wa kusafirisha maji kwenye miundombinu ya umwagiliaji unaomilikiwa na kuhudumiwa na Serikali au vyama vya umwagiliaji sipokuwa mkaguzi wa umwagiliaji au mtu yote aliyepewa mamlaka hayo.
Sheria hiyo ya umwagiliaji inazuia kuvua katika mabwawa yanayomilikiwa na kutunzwa au kusimamiwa na Serikali au vyama vya umwagiliaji bila kibali cha maandishi kutoka kwa mkaguzi wa umwagiliaji isipokuwa kwa masharti na vigezo na kulipa ada kama itakavyopangwa .
Marufuku kutumia milipuko au kitu chochote cha sumu kwa madhumuni ya kuvua katika bwawa.
Bila kibali cha maandishi cha Tume kuchimba madini au kufanya shughuli kwa kutumia mlipuko au shughuli yoyote inayoweza kusababisha mtikisiko ndani ya umbali wa kilometa moja kutoka kwenye skimu.
Ni marufuku kuruhusu maji kutoka katika miundombinu ya umwagiliaji inayomilikiwa, kusimamiwa au kutunzwa na Serikali au vyama vya umwagiliaji kwa kukatwa tuta au kutoboa, kujeng mlango au kwa njia nyingine zinazofanana na hizi.
Marufuku kuunganisha mifereji au bomba kwenye mfumo wa umwagiliaji matupio na kutoweka au kusababisha kuweka umbo au kuweka kidaa katika mfereni au bomba ilitounganishwa kwenye mifumo ya umwagiliaji na matupio.
Picha zote ni za Uzinduzi wa Taasisi ya Tanzania Youth Agro Irrigation Development Network Programme uliofanyika Ofisi ya mkuu wa mkoabwa Mara.
Post a Comment