RC CHALAMILA KUONGOZA MBIO ZA HISANI ZA TCAA
Na Andrew Chale, Dar es Salaam
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila anatatarajiwa kuongoza mbio za hisani za miaka 20 ya Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) zitakazofanyika Oktoba 29,2023 katika Viwanja vya Mlimani city majira ya saa 12 asubuhi.
Mbio hizo ni maalum kusaidia mapambano ya hali ya ukame katika maeneo ya Nchi ikiwemo Dodoma, Kilimanjaro na mengine ambapo mbio za KM 5 na 10 wananchi na wadau wa TCAA watakimbia.
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Oktoba 26,2023, Mwenyekiti wa Maadhimisho hayo Mellania Kasese amesema mkuu wa mkoa Albert Chalamila ataongoza washiriki zaidi ya 400.
Kasese amesema maandalizi ya mbio hizo tayari yamekamilika. Katika mbio hizo za hisani zitaanzia katika ruti ya kilometa tano mpaka kumi hivyo aliwaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi.
"Shamra shamra za Maadhimisho haya zimekuwa zikiendelea yakiendelea lengo likiwa kuzungumzia mafanikio yaliopatikana katika miaka hiyo 20 mpaka sasa maandalizi yamekamilika vifaa vyote vimeishawasili.
Aidha amesema lengo kuu la mbio hizo ni kuunga mkono jamii iliyoko katika maeneo ya ukame ili iweze kupanda miti ya kutosha ili kupunguza uhalibifu wa hali ya hewa.
Naye katibu wa Chama Cha riadhaa mkoa wa Dar es salaam , Samweli Mwela abainisha kuwa, tangu awali wamekuwa walishirikiana na TCAA katika maandalizi y mbio hizo wamekuwa walishirikiana vyema katika maandalizi kutokana na Chama hicho ndio limekuwa kikiusika katika mbio zote.
Post a Comment