HEADER AD

HEADER AD

TIMU 8 ZAFUZU ROBO FAINALI MASHINDANO YA ESTER BULAYA CUP 2023

Na Shomari Binda, Bunda

TIMU 8 zimefanikiwa kufuzu hatua ya  robo fainali ya mashindano  ya Ester Bulaya Cup 2023 yanayoendelea mjini Bunda.

Mashindano hayo yaliyoanza mwishoni mwa mwezi uliopita kwa kushirikisha timu 20/yamekuwa yakiwavutia watu wengi na kujitokeza kwenye uwanja wa sabasaba.

Timu zilizoguzu kwenye hatua hiyo ni Amani fc,Kabasa fc,Bunda kids,Kung'ombe fc,Bunda yosso,Sazira fc,Bunda boma na Kunzugu fc.

            Ester Bulaya akizungumza na wachezaji

Hatua ya robo fainali inatarajiwa kuanza kutimua vumbi oktoba 23 ambapo ushindani unatarajiwa kuonekana kwenye kila mchezo.

Mmoja wa mashabiki wa soka mjini Bunda Juma Muya amesema mashindano hayo yamekuwa na burudani na kumpongeza muandaji wa mashindano hayo mbunge wa viti maalum Ester Bulaya.

Amesema burudani hiyo ilikosekana kwa muda na wakati huu wamepata mahala pakwenda kuangalia michezo mbalimbali.

" Tunapenda kumshukuru mbunge Bulaya kwa kuturejeshea burudani hii ambayo tulikuwa tumeikosa kwa muda mrefu",amesema Muya.

Akizungumza na DIMA ONLINE muandaaji wa mashindano hayo mbunge wa viti maalum Ester Bulaya amesema kwa namna wananchi wanavyojitokeza kwa wingi kwenye mashindano hayo sasa yatafanyika kila mwaka.

Amesema siku ya fainali ya mashindano hayo kutafanyika na michezo mingine ikiwemo ya mpira wa miguu ya timu za wanawake na walemavu pamoja na mchezo wa draft.

No comments