HEADER AD

HEADER AD

ZIFF, EU NA UONESHAJI WA FILAMU MIKOA MITATU YA TANZANIA BARA

Na Andrew Chale, Dar es Salaam

TAMASHA la Kimataifa la filamu za Nchi za Majahazi (Zanzibar International Film Festival-ZIFF) kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU), Nchini wametangaza rasmi uoneshaji wa filamu katika Vyuo Vikuu kwenye mikoa mitatu ya Tanzania Bara linalokwenda kwa jina la “ZIFF Goes Mainland 2023”.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa ZIFF aliyemaliza muda wake ambaye anaratibu mpango huo, wa "ZIFF Goes Mainland 2023" amesema mpango huo umeendelea kuimarika  na kuanzia Novemba 3, 2023, filamu tano zilizoshinda tuzo kutoka msimu wa 26 wa ZIFF na filamu teule za Ulaya zitaonyeshwa.

‘’Filamu hizi zitaoneshwa katika Mikoa ya Dar es Salaam ikiwemo Chuo cha Kampala KIU, Pwani Wilaya ya Bagamoyo katika Chuo cha TaSUBa, na Morogoro katika chuo kikuu Mzumbe. Wanafunzi watashiriki katika majadiliano baada ya kutazama kuhusu filamu na mbinu zao za kutengeneza filamu.

Tamasha hilo litafungua filamu ya "EONII" ya mwongozaji Mtanzania, na pia kutakuwa na filamu kutoka nchi za Ulaya kuangazia utofauti wa kitamaduni tajiri.’’ Amesema Prof. Martin Mhando.

Aidha, Mwaka huu, ili kuonyesha mshikamano kati ya vita vinavyoendelea na Urusi, filamu kutoka Ukraine, Pia filamu kutoka Afrika Kusini, Kenya, Misri na Tanzania.

‘’TeamEurope - EU, taasisi zake na nchi wanachama - imekuwa muhimu katika kuimarisha tamasha la ZIFF.

Ushirikiano wetu na shughuli za zamani ikiwa ni pamoja na kusaidia warsha za mafunzo, kufadhili programu za ZIFF, ili kuwasilisha fursa za utayarishaji wa pamoja”. Amesema Prof. Martin Mhando

Kwa upande wake, Mkuu wa Ujumbe wa EU nchini Tanzania, Mhe. Balozi Bi. Christine Grau amesema; "Ulaya imechangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa tamasha zaidi ya kuonyesha filamu binafsi. Kusaidia wadau wanaohusika na utamaduni, na kuanzisha miundomsingi inayosaidia wasanii kujitahidi na kuhamasisha jamii zao.

Katika mkutano huo, wawakilishi kutoka Balozi tisa zikiwemo nchi za Spain, Belgium, Germany, Ireland, France, Poland, Finland, Italy na Sweden zinazochangia mpango huo wa ZIFF kwenda Bara 2023 wameweza kuhudhuria, wakisisitiza ari ya #TeamEurope na jukumu la Diplomasia ya kitamaduni katika kukuza amani katika Ulaya na Afrika.

Baadhi ya filamu hizo tano ni pamoja na N8, MWANDISHI,NEB TAWY,  9MEMEZA na EONII.

No comments