WANANCHI KATA YA BWERI WASEMA UBORESHAJI KITUO CHA AFYA NI MUHIMU
Na Shomari Binda, Musoma
WANANCHI wa Kata ya Bweri Manispaa Musoma mkoani Mara, wamesema uboreshaji wa kituo cha afya Bweri ni Muhimu sanjari na upatikanaji wa vifaa tiba.
Wamesema eneo la Bweri lina wakazi wengi wanaokitumia kituo hicho hivyo kinahitaji vifaa tiba pamoja wataalamu wa kuwahudumia.
Wakizungumza wakati wakifatilia kikao cha kwanza cha mkutano wa 13 wa bunge la 12 eneo la Kariakoo wamesema kituo hicho kina umuhimu mkubwa hivyo kinahitaji maboresho
Phinias Nyadundo mkazi wa Songamele amesema kituo hicho ni msaada mkubwa kwao lakini bado baadhi ya huduma zimekuwa hazipatikani licha ya kuwa ni cha muda mrefu.
Phinias Nyadundo mkazi wa SongameleMkazi wa Morembe Kata hiyo ya Bweri Godfrey Machumu amesema kutoka Morembe kwenda hospital ya wilaya kuna umbali hivyo kituo cha karibu cha msaada wa haraka ni Bweri
Charles Isaya amesema kituo cha afya Bweri ni cha muda mrefu na kinahitaji kuongezwa majengo na vifaa tiba ili kiendelee kutoa huduma.
Charles Isaya mkazi wa Kata ya BweriNdiga Odongo mkazi wa Kariakoo amesema kituo hicho kikiboreshwa na kuwepo na vifaa tiba vya kutosha itakuwa msaada kwao wa huduma za afya.
" Sisi kama bodaboda tunapopata changamoto kwenye shughuli zetu hata huduma ya kuongezewa damu inachukua muda kwa kuwa hakuna benki ya damu kituoni"amesema Juma Kogaro.
Wamemshukuru mbunge wa jimbo la Muso mjini Vedastus Mathayo kwa kuomba fedha serikalini kwaajili ya kituo chao cha afya.
Mmoja wa wananchi wa Kata hiyo Bweri Athuman Kitwara amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Musoma amesema mbunge Mathayo kuomba fedha serikarini kupitia Tamisemi ili kukiboresha anajua umuhimu wake.
Amesema afya ni suala la msingi na pale mwananchi anapokuwa na afya njema anaweza kufanya shughuli za kiuchumi.
" Kituo hiki kina umuhimu mkubwa na kinawahudumia watu wengi tunamshukuru mbunge Mathayo kuomba fedha kwaajili ya maboresho"amesema Kitwara.
Katika kikao cha Oktoba, 30,2023 kikao cha kwanza cha mkutano wa 13 wa bunge la 12 mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo aliuliza swali la nyongeza TAMISEMI ni lini itapeleka fedha kwaajili ya kituo cha afya Bweri kwaajili ya maboresho ya kituo hicho.
Akijibu swali la mbunge huyo Naibu Waziri wa TAMISEMI Dk.Festo Dugange amesema kituo hicho ni cha kimkakati na serikali itatenga fedha kwaajili ya kituo hicho.
Mkazi wa Kata ya Bweri Anastazia ambaye ameomba kituo cha afya Bweri kuboreshwa.
Post a Comment