HEADER AD

HEADER AD

BUNDA SPORTS KIDS MABINGWA ESTER BULAYA CUP 2023, MDEE ANUNUA MAGOLI

>> Bunda Sports yajinyakulia Milioni 2

>> Mshindi wa pili Sazira FC ukiondoka na  Milioni moja

Na Shomari Binda, Bunda

TIMU  ya  Bunda  Sports Kids  wamekuwa mabingwa wapya wa mashindano ya Ester Bulaya Cup 2023 baada ya kuifunga timu ya Sazira fc mabao 3-0

Mgeni rasmi kwenye fainali hiyo mbunge wa viti maalum Halima Mdee kabla ya kuanza mchezo huo wa fainali alitangaza kununua kila gori litakalofungwa kwa shilingi laki 1.

     Kushoto ni Mbunge Halima Mdee ,kulia ni Mbunge Ester Bulaya 

Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi ikiwa ni vikombe na fedha taslim,Mdee amesema namna mashabiki wengi walivyojitokeza ni imani wameyapokea mashindano hayo.

Amesema michezo ni ajira kubwa katika kipindi hiki na kumpongeza mbunge Ester Bulaya kwa ubunifu wake na kuanzisha mashindano makubwa.

Amesema kwa taarifa alizonazo wapo wachezaji waliopitia mashindano hayo tangu yaanzishwe ambapo wanacheza ligi kuu na kudai ni mafanikio ya mashindano hayo.


Nikushukuru sana pacha wangu kwa kuanzisha mashindano haya ambayo yameonyesha mafanikio makubwa tangu yalipoanza kufanyika.

" Kabla ya mchezo kuanza niliahidi kununua kila goli kwa laki moja naomba niwapongeze wafungaji na  waje niwakabidhi pesa zao hapa hapa",amesema Mdee.

Kwa upande wake muandaaji wa mashindano hayo mbunge wa viti maalum Ester Bulaya amesema kumalizika kwa mashindano hayo ni mwanzo wa kuanza mashindano mengine.

Bulaya amewapongeza washindi wa michezo mbalimbali na kuzitaka timu zote kuendelea na mazoezi kwasjili ya mashindano mengine na kudai wachezaji waliotokea Ester Bulaya wanacheza nje ya nchi.

" Niwapongeze washindi wote wa mwaka huu lakini niwaambie kumalizika kwa mashindano haya ni mwanzo wa kuanza kwa mashindano mengine",amesema Bulaya.

Kwa kuchukua ubingwa huo timu ya Bunda Sports Kids imepata kikombe na fedha taslim  Tsh Milioni mbili huku mshindi wa pili timu ya Sazira ikiondoka na Tsh. Milioni moja.

       Bunda Sports Kids mabingwa Ester Bulaya Cup 2023

Zawadi nyingine zilizotolewa ni kwa mabingwa wa soka la wanawake timu ya Bunda Queen iliyoifunga timu ya Bunda Kids mabao 3-1 pamoja na washindi wa mchezo wa draft,karata,bao,mbio za baiskeli kwa wenye ulemavu.

No comments