HALMASHAURI SERENGETI YAWAOMBA WAKULIMA KUFIKA KUNUNUA MBOLE YA KUKUZIA KWA BEI NAFUU
Na Shomari Binda, Serengeti
WAKULIMA wilayani Serengeti wametakiwa kufika maeneo yanayouza mbolea ili kuinunua kwaajili ya kukuzia mahindi.
Wito huo umekuja baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kupokea shehena ya mbolea ya ruzuku kutoka serikalini.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Kaimu Mkurugenzi wa halmashsuri hiyo Bwenda Bainga amesema mbolea ipo ya kutosha na kuwataka wakulima kuitumia fursa hiyo.
Amesema serikali inawathamini wakulima hapa nchini kwa kuwajali pembejeo na mbolea ili kukuza kilimo chao.
Bainga amesema mbolea ya ruzuku inapatikana kwa bei nafuu na kuwaita wakulima maeneo husika ili kupata mbolea hiyo.
Kaimu Mkurugenzi huyo ambaye pia ni afisa kilimo wa halmashauri hiyo ya Serengeti amesema licha ya wakulima kuhamasishwa kupata mbolea hiyo ya kukuzia lakini pia wanawapa elimu ya matumizi yake.
" Tumepokea mbolea ya ruzuku ya kutosha na tunawaomba wakulima wafike maeneo husika ili waweze kununua mbolea hiyo kwa gharama nafuu.
" Tumejipanga pia kuwapa elimu wakulima wetu juu ya matumizi sahihi ya mbolea ya kukuzia na wapate mazao yenye tija",amesema Bainga.
Baadhi ya wakulima wameishukuru serikali kwa mbolea ya ruzuku kwaajili ya kukuzia mazao na kuahidi kufika maeneo husika ili kununua.
Post a Comment