MAKONDA KUZUNGUMZA NA WAZEE CCM MUSOMA
KATIBU wa Halmashauri kuu, Itikadi, Ueneze na Mafunzo Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Paul Makonda anatarajiwa kuzungumza na Wazee wa Musoma mkoani Mara
Makonda atafanya mazungumzo katika ukumbi wa CCM mkoa wa Mara majira ya saa nne asubuhi, Novemba, 14, 2923 kisha kuelekea wilayani Tarime ambako atafanya mkutano wa hadhara.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na ziara ya kiongozi huyo mkoani Mara, Katibu wa Siasa Uenezi na Mafunzo mkoa wa Mara Simon Rubuga amesema maandalizi ya mapokezi ya kiongozi huyo yamekamilika.
Amesema Makonda anatarajiwa kupokelewa Novemba 13 majira ya saa 9 alasiri wilayani Bunda na kuelekea wilayani Butiama.
Rubuga amesema akiwa Butiama kiongozi huyo ataweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na baadae kuzungumza na familia yake.
Amesema baada ya kutoka Butiama atapumzika mjini Musoma kabla ya kuendelea na ziara Novemba 14 mkoani Mara.
Amesema kiongozi huyo katika siku yake ya pili atafanya kikao na Kamati ya Siasa ya mkoa kisha kuzungumza na wazee mjini Musoma kwenye ukumbi wa CCM.
Mara baada ya kuzungumza na wazee hao atatembelea maeneo kadhaa ya mji wa Musoma na baadae kuelekea wilayani Tarime kwaajili ya mkutano wa hadhara.
" Niwaombe wanachama wa CCM na wananchi wote kujitokeza kumpokea na kumsikiliza kiongozi huyo kwenye maeneo yote atakayopita.
" Ameamua kuanzia ziara yake Kanda ya ziwa tangu amechaguliwa hivyo ni muhimu kujitokeza kumpokea kwa kishindo kama walivyofanya maeneo mengine ambayo ameshapita",amesema Rubuga.
Post a Comment