WANAWAKE WAISHUKURU WORLD VISION KUJENGA JENGO LA MAMA NA MTOTO KUWANUSURU KUTEMBEA KM 24
BAADHI ya akina mama wa Kijiji chaKijiji Nkiniziwa katika Kata ya Nkiniziwa wilaya ya Nzega mkoa wa Tabora wamelishikuru Shirika la World Vision kuwajengea jengo la kujifungulia ambalo litawapunguzia kutembea mwendo wa kilomita 24 kufuata huduma ya kukifungua Kituo cha afya Busondo
Mkuu wa wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Naitapaki Tukai amelipongeza Shirika la World Vision kwa kutekeleza mradi wa kujenga miundombinu ya huduma za Afya kwa kujenga jengo la kujifungulia kwa akinamama katika zahanati ya Nkiniziwa iliyoko wilayani humo.
Dc Tukai amesema hayo Novemba 15 mwaka huu wakati akizindua jengo hilo lililojengwa na Shirika la World Vision kupitia Mpango wa Maendeleo ya Jamii Ndala(Ndala AP) ambalo lina vyumba vitatu ikiwemo sehemu iliyotengwa kwa ajili ya kujifungulia akinamama ambayo pia ina vitanda kwa ajili ya kupatiwa huduma mara baada ya kujifungua.
Mkuu wa wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Naitapaki Tukai akizungumza na wananchi(hawapo pichani)wa kijiji cha Nkiniziwa wilayani humo katika viwanja vya ofisi ya Mradi wa World Vision Ndala AP.Mpango wa Maendeleo ya Jamii Ndala (Ndala AP)unajumuisha Kata tatu za Ndala,Nkiniziwa na Puge zenye jumla ya vijiji 11 na unatekeleza miradi ya Ufadhili wa Watoto,Miradi ya Sekta za Afya na Lishe,Maji na Usafi wa Mazingira,Kilimo,Mifugo na Uchumi pamoja na Ulinzi na Utetezi wa mtoto.
Amesema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inapenda kuona akinamama wanajifungulia kwenye maeneo salama ndiyo maana inawapa fursa hata Wadau mbalimbali wa maendeleo kuisaidia kama Shirika la World Vision lilivyofanya.
Vyoo vya kisasa vilivyojengwa na shirika la World Vision katika shule ya Msingi Kipugala wilaya ya Nzega mkoa wa Tabora.“Nimefurahi sana kuona wakinamama wakiwa na watoto wao mmejitokeza kwa wingi kufika kwenye eneo hili ili kuweza kushuhudia uzinduzi wa jengo hili na hii inadhihirisha mmefurahishwa na msaada huu uliotolewa na shirika hili la World Vision,”
“Kwanza niwapongeze World Vision kwa msaada huu waliotupatia wa kutujengea jengo hili ambalo ni muhimu sana kwa ajili ya akinamama kujifungulia,mimi kwa niaba ya Rais Dkt Samia Suluhu niwashukuru sana na leo ninalizindua na bahati nzuri usiku wa kuamkia leo amezaliwa mtoto mmoja katika jengo hilo,”amesema.
Amesema kuwa shirika hilo limekuwa likiisaidia serikali ya wilaya hiyo katika sekta mbalimbali zikiwemo za Elimu,Afya,Maji katika kuwahudumia wananchi hivyo amewaagiza Viongozi wa Serikali na Watendaji walioko kwenye miradi iliyotekelezwa kuakikisha wanashirikiana ili kuona miradi hii inatunzwa na kulindwa kwa manufaa ya umma.
Mkuu wa wilaya ya Nzega mkoani Tabora,Naitapaki Tukai(aliyesima wa kwanza kulia)akimkabidhi mmoja wa wahitimu cherehani baada ya kuhitimu mafunzo ya miezi mitatu ya ushonaji wa nguo yaliyoandaliwa na Shirika la Wolrd Vision Ndala AP.“World Vision wameshamaliza kazi yao suala la utunzaji kwa matumizi endelevu ni letu sisi watumiaji hivyo usimamizi wa karibu wa miradi hii kwenye maeneo yenu ni suala la msingi sana” alisisitiza Dc Tukai.
Ameongeza kuwa fedha zilizotumika kutekeleza miradi hiyo ni fedha ya ziada kutoka kwa Wananchi wa Ireland hivyo ni vema kuona thamani ya upendo wao kwa kulinda na kutunza majengo, na vifaa vyote vilivyonunuliwa kwa ajili ya miradi hii.
Awali Mratibu wa Mpango wa Maendeleo ya Jamii-Ndala(Ndala AP)Ngasa Michael akisoma taarifa ya Utekelezaji wa Miradi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 walipokea kiasi cha Shilingi Milioni 600 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi ukiwemo mradi huo wa ujenzi wa jengo hilo.
Mratibu wa Mpango wa Maendeleio ya Jamii-Ndala(Ndala AP)Ngassa Michael(aliyesimama)chini ya Shirika la World Visionakisoma taarifa fupi ya utekelezaji wa miradi kwa mwaka 2022/2023.Amesema kuwa wamekuwa wakipata ushirikiano mkubwa kutoka katika serikali ya wilaya hiyo wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo ndiyo maana wanafanikiwa na wataukabidhi mradi huo serikalini mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wake.
Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo,Gasper Ernest ameiomba serikali kuipatia vifaa tiba kwani kwa sasa ina upungufu mkubwa pamoja na upungufu wa nyumba za watumishi hali ambayo inawafanya wafanye kazi zao katika mazingira ambayo si rafiki sana.
Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Nkiniziwa,Gasper Ernest(wa kwanza kulia)akitoa taarifa ya kukamilika kwa jengo la kujifungulia kwa Mkuu wa wilaya ya Nzega mkoani Tabora,Naitapaki Tukai(wa kwanza kushoto).Pia amekabidhi vyoo vya kisasa na manawio ya mikono kwa ajili ya wanafunzi wa Shule za Msingi Nkiniziwa na Shule ya Msingi Kipugala miradi yote hii ni sehemu ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kupitia Mpango wa Maendeleo ya Jamii- Ndala(Ndala AP).
Mratibu wa Mpango wa Maendeleo ya Jamii Ndala,Ngasa Michael(mwenye miwani)ulioko chini ya Shirika la World Vision akizungumza mara baada ya kumkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Nzega,Naitapaki Tukai jengo la kujifungulia katika Zahanati ya Nkiniziwa.
Post a Comment