HEADER AD

HEADER AD

WCF WAJIVUNIA ONGEZEKO BILIONI 65 LA FIDIA KWA WANUFAIKA


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umejivunia ongezeko la fidia kwa wanufaika wake kutoka kulipa Bilioni 1.55 mwaka 2017 hadi kufikia kulipa Bilioni 65. 35 mwaka 2023.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma wakati wa kikao kazi Jijini Dar es Salaam katika muendelezo wa vikao chini ya msajili wa Hazina.

Amebainisha kuwa, Idadi ya madai ya fidia kwa wanufaika waliyopokelewa na mfuko huo ni 18,782 na jumla ya madai 14,087 yameshughulikiwa ambapo 12,339 yamelipwa, madai 1440 yamekataliwa na 308 yamefungwa.

Aidha Dkt. Mduma amesema wamefanikiwa kuimarika uwezo wa kifedha wa mfuko kwa shilingi Bilioni 697.83 kwa mujibu wa hesabu za mpaka tarehe 30 Septemba 2023.

Pia amesema wamefanikiwa kuboresha huduma kupitia usimikaji mifumo ya TEHAMA, Kuboresha kwa kituo Cha huduma kwa wateja na kuboresha tathmini za Ulemavu kupitia mafunzo kwa madaktari.

Kwa upande wa ukusanyaji michango, Dkt. Mduma amesema waajiri wote wanatakiwa kuchangia katika mfuko ambapo waajili Sekta Binafsi 0.5% na waajiri Sekta ya umma 0.5%.

Amesema mfuko huo hadi sasa umefanikiwa kulipa kiasi cha Tsh. bilioni 65 kwa wanufaika wake huku akiahidi kuendelea kuimarisha zaidi kwa maslahi ya watanzania na taifa kwa ujumla.

Amesema Hadi Sasa mfuko umetoa malipo ya kodi ya Serikali inayotokana na mapato kiasi Cha shilingi bilioni 62.7 huku akibainisha kuwa hadi kufikia September 2023 mfuko umesajili aslimia 93 ya wanufaika.

Akizungumza kwa niaba ya wahariri Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri TEF, Deodatus Balile amewataka Wahariri pamoja na waandishi wa habari kwenda kufikisha taarifa kwa waajiri wao ili wapate haki yao ya msingi ya kujiunga na mfuko huo.

Amewasihi mashuhuda waliopata changamoto na kulipwa fidia zao kuwa tayari kuzungumza na vyombo vya habari ili elimu ifikie Umma wa wananchi kwa kiasi kikubwa.




No comments