MBUNGE MASHIMBA NDAKI AGAWA MAJIKO YA GESI KWA MAMALISHE JIMBONI
Na Samwel Mwanga, Maswa
MBUNGE wa jimbo la Maswa Magharibi, Mashimba Ndaki amegawa majiko ya gesi 241 kwa Mama Lishe katika jimbo hilo lenye Kata 17 lililoko katika wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu kwa ajili ya kuhamasisha watumie nishati ya gesi kwa lengo la kutunza mazingira.
Pia katika makabidhiano hayo yaliyofanyika katika maeneo ya makao makuu ya Kata hizo ilitolewa elimu kuhusu matumizi ya majiko ya gesi ili yasiweze kuleta madhara kwa watumiaji.
Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi, Mashimba Ndaki(kulia aliyechuchumaa,) akikabidhi Mama Lishe,Gumba James wa Kijiji cha Masela jiko la gesi.Akizungumza katika maeneo mbalimbali na nyakati tofauti tofauti katika jimbo wakati wa akigawa majiko hayo kuanzia Desemba 30 hadi Desemba 31 mwaka huu amesema kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha wananchi kutumia gesi na nishati mbadala na kuacha kutumia mkaa na kuni ili kuepukana na uharibifu wa mazingira nchini.
Amesema kwa kipindi cha sasa kumekuwa na mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kusababisha athari mbalimbali zikiwemo kuwepo kwa upungufu wa mvua unaotokana na shughuli za kibinadamu zikiwemo kukata miti kwa ajili ya kuchoma mkaa na kuni kwa ajili ya kupikia.
Mama Lishe,Kundi Cherehani wa Kijiji cha Bukangilija akipokea jiko la gesi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi,Mashimba Ndaki“Tunamsaidia Rais Samia Suluhu Hassan kuhamasisha matumizi ya gesi na nishati mbadala nawaomba mama Lishe mtumie nishati ya gesi na nishati mbadala kama vile umeme muwache kutumia mkaa na kuni ukataji miti ovyo nchi yetu itakuwa janga ni uharibifu wa mazingira “
“Haya majiko ya gesi ninayagawa bure na hii mitungi yake ni ya kudumu ni vizuri mkaitumia vizuri mkumbuke hii ni gesi hivyo hata kama una mtoto wako au msaidizi wako ni vizuri ukamuelekeza jinsi ya kulitumia kama mlivyopatiwa elimu ili lisiweze kuleta madhara kwa mtumiaji na gesi ikiisha ni vizuri muende mkajaze ni gharama nafuu ukilinganisha na matumizi ya mkaa,”amesema.
Mbunge Mashimba amewataka Mama lishe hao katika jimbo hilo kuungana kwa pamoja na kuunda SACCOSS ambayo itawasaidia kuinua mitaji yao ili biashara yao iwe endelevu na kuwahaidi iwapo wataanzisha hiyo Saccos atawaongezea kiasi cha Sh Milioni 10.
Mama Lishe,Kundi Cherehani wa Kijiji cha Bukangilija akipokea jiko la gesi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi,Mashimba NdakiAidha amesema matumizi ya gesi ni salama kwa afya, mtu anapotumia hawezi kupata hewa chafu matumizi yake ni salama kiafya tofauti na kuni ambazo zikitumiwa muda mrefu na umri unapokwenda hasa kwa wakinamama na macho yao yanakuwa na rangi nyekundu na hivyo kudhaniwa kuwa ni wachawi hasa katika maeneo hayo ya mkoa wa Simiyu na baadhi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Baadhi ya akina mama lishe wamempongeza Rais Dkt Samia Suluhu na Mbunge Mashimba Ndaki kwa kuwawezesha kupata majiko hayo na kuhaidi kuwa mabalozi wazuri katika kutoa elimu juu ya utunzaji wa mazingira hasa ukataji wa miti kwa ajili ya kuchoma mkaa pamoja na kuni kwa ajili ya kupikia na badala yake watu watumie nishati mbadala ikiwemo gesi.
Baadhi ya mama Lishe katika Kata ya Malampaka wakimdikiliza Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi,Mashimba Ndaki(hayupo pichani)kabla ya kukabidhiwa Majiko ya gesi.“Tunamshukuru sana Rais Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na Mbunge wetu Mashimba Ndaki kwa kutuona sisi mamalishe na kutupatia haya majiko ya gesi bure maana wengi tusingeweza kumudu kutoa kiasi cha Sh 50,000/=kwa ajili ya kununua hili jiko la gesi.
"Haya majiko yataturahisishia mapishi yetu hasa kwenye biashara zetu na tutakuwa mabalozi wazuri kutoa elimu juu ya athari ya ukataji wa miti hovyo kwa ajili ya kuchoma mkaa na kukata kwa ajili ya kuni za kupikia ,”amesema Mary Evarist ambaye ni Mamalishe na mkazi wa kijiji cha Kadoto.
Naye Magdalena Joseph ambaye ni mamalishe na mkazi wa kijiji cha Mwanundi alihaidi kulitunza jiko hilo sambamba na kulitumia kulingana na elimu ambayo amepatia juu ya matumizi sahihi ya jiko la gesi ili kuepuka madhara ambayo yanaweza kujitokeza.
Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi,Mashimba Ndaki(wa nne kutoka kulia)akiwa kwenye picha ya pamoja na Mama Lishe wa Kata ya Badi kabla ya kuwagawia majiko ya gesi.“Hili jiko la gesi ambalo nimepatiwa leo nahaidi nitalitunza vizuri na pia nitalitumia vizuri kutokana na elimu ambayo tumepewa juu ya matumizi sahihi ya jiko la gesi ili liweze kuninufaisha pamoja na kutosababisha madhara kwa mtumiaji,”amesema.
Sabina Daud ni Mamalishe wa kijiji cha Jija amesema kuwa kupitia jiko la gesi litamrahisishia shughuli ya mapishi na kumpunguzia muda tofauti na alivyokuwa akitumia jiko la mkaa.
Amesema gharama aliyokuwa akiitumia kwenye mkaa sasa ataipeleka kwenye mtaji ili aweze kukuza biashara anayofanya ya mgahawa.
Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi,Mashimba Ndaki(wa nne kutoka kulia)akiwa kwenye picha ya pamoja na Mama Lishe wa Kata ya Badi kabla ya kuwagawia majiko ya gesi.Majiko yaliyogawiwa kwa mama lishe ni katika Kata ya Zanzui (5), Mwamashimba (11) ,Buchambi(12),Kadoto(11),Shishiyu(11),Jija(9),Nyabubinza(13) na Mwanghonoli(9).
Kata nyingine ni pamoja na Mwabayanda (5) ,Kulimi(5) ,Busangi(14) ,Sengwa (18) ,Masela(24),Isanga(21),Badi(20),Mataba(11)na Malampaka (42).
Post a Comment