Home
/
HABARI KITAIFA
/
RC MTANDA ASEMA BILIONI 18.5 ZA SERIKALI ZIMESAIDIA KUTATUA CHANGAMOTO VYUMBA VYA MADARASA

Na Dinna Maningo, Mara
Mkuu huyo wa mkoa ameyasema hayo Desemba, 30, 2023 katika kikao cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa.
Mkuu wa mkoa wa Mara Said Mtanda
Kikao hicho kilifanyika kwa njia ya Zoom kilichorushwa mbashara katika Televisheni ya Taifa TBC ambapo kila mkuu wa mkoa alisoma taarifa ya ujenzi wa miradi ya elimu iliyotolewa fedha na serikali.
Lengo la kikao hicho TAMISEMI ilitaka kufahamu kila mkoa umefikia hatua gani katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na vyoo na kwa namna gani mikoa hiyo imejipanga kuhakikisha wanafunzi wa awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza wanajiunga na masomo.
RC Mtanda amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na TAMISEMI kwa kuupatia mkoa wa Mara fedha Bilioni 18.5 kupitia mradi wa BOOST na SEQUIP ambazo zimetumika kujenga shule mpya, vyumba vya madarasa , mabweni na matundu ya vyoo.
Mtanda amesema kuwa wanafunzi watajiunga na masomo na kwamba hakuna mwanafunzi atakayeshindwa kujiunga na masomo ya awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza kutokana na ukosefu wa madarasa.
"Kati ya fedha hizo Bilioni 12.7 ni za mradi wa Boost, shule 17 za msingi zenye vyumba 224 zimeshakamilika. madarasa 18 ya awali, matundu ya choo 144, madarasa maalum 2 yamekamilika.
"Tumekamilisha shule 10 za sekondari na shule moja ya bweni ya wasichana wilayani Bunda ya Bilioni 3, vyumba vya madarasa 46 vimekamilika, mabweni 11 yamekamilika na matundu ya vyoo 68" amwsema RC Mtanda.
Ameongeza kusema" Tunaendelea kukamilisha shule ya Songe, kwa Tarime DC shule ya Borega hasa mabweni mawili yaliyokuwa yamesalia ukamilishaji wake"alisema Mtanda.
" Kwa uwiano wa 1 kwa 50 mahitaji ya vyumba vya madarasa katika mkoa wa Mara ni 1,148, hadi sasa tunavyo vyumba 1,009 , tofauti ni vyumba 139.
"Katika mkoa wetu tuna maboma 154 katika halmshauri zote tisa na yanaendelea kufanyiwa kazi na ifikapo Januari, 2024 vyumba vyote vitakuwa vimekamilika.
Akizungumzia zoezi la uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la awali 2024 amesema wameweka lengo kuandikisha wanafunzi 74, 234 na hadi Desemba, 2023 wameshaandikisha wanafunzi darasa la kwanza 49,964 sawa na asilimia 67 na uandikishaji unaendelea.

Wakuu wa mikoa wakiwa kwenye kikao na Waziri TAMISEMI kilichofanyika kupitia Zoom video.
Aidha kwa darasa la awali wamekwisha andikisha wanafunzi 44,835 sawa na asilimia 54.2 na kwa mwaka 2023 wanafunzi 70, 134 walifanya mtihani katika mkoa huo, kati ya wanafunzi hao 52,722 sawa na asilimia 76.04 walifaulu mtihani na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.
RC Mtanda amesema shule 18 za Kata zimesajiliwa na shule 2 katika mkoa huo hazijasajiliwa, moja ipo wilaya ya Butiama na nyingine Serengeti na kwamba taratibu zote zimekamilika na wataalam wameshawasilisha nyaraka TAMISEMI.
Amewashukuru wakuu wa Wilaya zote na Wakurugenzi wa halmashauri, Katibu Tawala mkoa wa Mara, wilaya , Idara ya Elimu na Wabunge kwa usimamizi wa miradi katika sekta ya elimu kwani yeye pekee asingeweza.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa amewapongeza wakuu wa mikoa kwa kazi wanayoifanya kwani taarifa walizozitoa ni za matumaini kwa watanzania na wananchi ambao wapo katika mikoa yao.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa.
"Kwakuwa mmeweka miadi katika maeno ambayo bado mchakato wa ujenzi unaendelea kuwa tarehe 15 mwezi Januari majengo yatakamilika na watoto wataenda shule. Hakikisheni majengo yanakamilika kama mlivyoahidi" alisema Mchengerwa.
Amesema baada ya tarehe hiyo yeye na wasaidizi wake watapita kila mkoa, wilaya na halmashauri kukagua miradi mbalimbali hasa miradi ya elimu.
Pia Waziri huyo amewaelekeza wakuu wote wa mikoa kuhakikisha shule zote zinasajiliwa hasa shule za wasichana na zianze kupokea wanafunzi.
Amewataka wakuu wa mikoa kuhakikisha wanasimamia usajili wa wanafunzi wanaojiunga na elimu ya awali, darasa la kwanza lakini pia kuhakikisha wanasimamia mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza na kuhakikisha kunakuwa na mahudhulio kwa wabafunzi wote bila masharti.

Post a Comment