HEADER AD

HEADER AD

WANANCHI TARIME WATAKIWA KUWAFICHUA WEZI WA TAA ZA BARABARANI


Na Dinna Maningo, Tarime

MENEJA Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) , Wilaya ya Tarime Mkoani Mara, Mhandisi Charles Marwa amewaomba wananchi kuwafichua wezi wa Taa za barabarani

Akizungumza na DIMA Online, Meneja TARURA, amesema kumezuka wizi wa taa za barabarani lakini wananchi hawatoi taarifa dhidi ya wanaohujumu miundombinu ya barabara jambo ambalo linarudisha nyuma jitihada za serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi.

      Meneja Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) , Wilaya ya Tarime Mkoani Mara, Mhandisi Charles Marwa

"Kuna sehemu mbalimbali kumeibuka wizi wa taa za barabarani mtu anakatia chini kabisa anaiba betri na sola na maeneo zilipo taa hizo ni barabarani ni karibu na makazi ya watu wanapita lakini uhalifu unafanyika watu wanakaa kimya wanawaficha wahalifu hawawasemi.

"Niwaombe wananchi wa Tarime pale ambapo mmoja wetu ataonekana anahujumu basi najua eneo hilo wapo wananchi tusiwafiche tutoe taarifa na ikiwezekana tuwakeme tujitahidi kuitunza na kuipenda miundombinu ya barabara inamanufaa kwetu sote " amesema Meneja TARURA.

Mhandisi Charles amesema tayari mikakati imewekwa kwa kushirikiana na Polisi kuhakikisha wahalifu wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria na kushtakiwa kwa kosa la uhujumu uchumi.

Baadhi ya Wananchi Tarime wamesema kuwa kitendo cha kuiba taa za barabarani kisifumbiwe macho kwani kinarudisha nyuma jitihada za serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.

           Taa iliyoibwa betri eneo la darajani unapoingia Tarime mjini.

Mkazi wa Mtaa wa Rebu Sokoni Mariam Tura amesema "Wananchi tushirikiane kulinda taa za barabarani tusiwafiche wahalifu tuwataje ili wachukuliwe hatua kukomesha huu wizi.

"Kabla ya hizi taa za barabarani kuwekwa tulikuwa tunaogopa kutembea barabarani nyakati za usiku maana kulikuwa ni giza na vibaka walikuwa ni wengi.

" Taa zilipowekwa zimesaidia uhalifu ukapungua kutokana uwepo wa mwanga barabarani lakini wizi umeanza kitendo kitakachosababisha giza na vibaka watarejea maeneo ya barabarani tutaporwa pesa, simu na mali zingine" amesema Mariam.

Mwita Chacha Mkazi wa mtaa wa Mwangaza ameomba ikiwezekana baadhi ya maeneo yenye taa za barabarani ziwekwe kamera ili kusaidia kulinda taa za barabarani.

        Taa ya Barabarani inayotumia umeme wa jua (Sola)

"Mara nyingi wizi hutokea nyakati za usiku sana watu wakiwa wameshalala hawapiti barabarani, kugundua kuwa fulani ndio kaiba ni vigumu sana.

"Labda itokee mtu huyo aliyeiba kaenda kuuza,basi tunaomba anayeuziwa atoe taarifa Polisi maana taa hizi ni faida kwa watu wote katika kulinda usalama wao na pindi wanapokuwa wakifanya shughuli zao za biashara taa zinasaidia wanapata mwanga.

Wananchi wameiomba Serikali kutumia kila mbinu kuwabaini wezi wa taa na iwachukulie hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa watu wenye nia ovu ya kufanya uhalifu huo.

Amesema vingineyo wizi wa taa za barabarani utakuwa sugu utakaoigharimu serikali kuweza kutoa fedha mara kwa mara kuweka taa za barabarani.

No comments